Habari Rfi-ki

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 3:59:44
  • More information

Informações:

Synopsis

Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

Episodes

  • Mada huru ya mwisho wa mwaka 2025

    26/12/2025 Duration: 10min

    Makala hii ya habari rafiki rafiki ijumaa ya desemba 26 2025 ni siku ya mada huru; tunakupa fursa kuchangia suala lolote ambalo limejiri nchini mwako wiki hii. Unaweza pia kuzungumzia kile ambacho umekisikia kwenye matangazo yetu ya redio juma hili. Nahodha wa Habari Rafiki Ruben Lukumbuka, moja kwa moja kutoka Studio maridai namba2.

  • Ulimwengu washerehekea sikukuu ya Krismasi

    25/12/2025 Duration: 10min

    Wakristo wanaadhimisha sikukuu ya Krismasi, wakati baadhi ya nchi kama Sudan, Ukraine na Mashariki mwa DRC yakikabiliwa na changamoto za usalama.-Unaadhimsisha sikuu ya Krismasi ukiwa wapi ? Sikukuu ya mwaka huu ikoje ?

  • Maandalizi ya timu za mataifa ya Afrika mashariki na kati katika AFCON 2025

    23/12/2025 Duration: 10min

    Msikilizaji Mashindano makubwa zaidi ya soka barani Afrika, Kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 yanaingia katika siku yake ya tatu leo jumanne ambapo jumla ya timu 24 za mataifa ya Afrika zikiwania taji hilo. Leo DRC wanamenyana na Benin, Tanzania wanakutana na Nigeria. Unazungumziaje maandalizi ya nchi za Afrika Mashariki na kati ?Nini matarajio yako kwenye mashindano haya ?

  • Tume ya umoja wa mataifa nchini DRC, MONUSCO yaongezewa mwaka mmoja zaidi

    22/12/2025 Duration: 10min

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa mwaka mmoja kwa ujumbe wa kulinda amani nchini DRC, wakati mapigano yakiongezeka mashariki mwa nchi hiyo kufuatia mashambulizi mapya ya waasi wa M23. Uamuzi huu unakuja wakati mjadala ukiendelea kuhusu ufanisi wa MONUSCO nchini humo. Je, unaamini hatua hii itasaidia au ujumbe huo umepoteza uaminifu na uwezo wa kuleta mabadiliko ya kweli? Je, umoja wa Mataifa unapaswa kufikiria upya mkakati wake wa kulinda amani nchini DRC?

  • Marekani yapiga marufuku kwa raia kutoka mataifa kadhaa kuingia ardhi yake

    18/12/2025 Duration: 10min

    Makala hii imeangazia hatua ya hivi karibuni ya rais wa marekani Donald Trump ya kuongeza orodha mpya ya mataifa zaidi yakiwemo ya Afrika ikiwemo Tanzania,  ambayo raia wake wanazuiwa kuingia Marekani, tumekuuliza Je? hatua hii ni ya kibaguzi ama inalenga kuulinda usalama wa Marekani? Na kwa mtazamo wako Hatua hii Ina maana gani? Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kupata maoni ya wasikilizaji

  • Waasi wa AFC/M23 watangaza kujiondoa katika mji wa Uvira DRC

    17/12/2025 Duration: 10min

    Kumekuwa na hisia mseto tangu waasi wa AFC/M23 wanaoungwa mkono na Rwanda watangaze kuwa watawaondoa wapiganaji wao katika mji wa Uvira mkoani Kivu Kusini mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Je? shinikizo la Marekani litazaa matunda? sikiliza maoni ya wasikilizaji wetu katika makala hii ya Habari rafiki 

  • Ukoloni mamboleo na maendeleo ya bara la Afrika

    15/12/2025 Duration: 09min

    Tarehe 14/12 dunia iliadhimisha miaka 60 ya azimio la kupinga ukoloni. Hata hivyo ukoloni katika sura zake za zamani na mpya bado unaathiri jamii zetu leo hii, baadhi wanaita ukoloni mamboleo.Je, ukoloni uliisha kweli Afrika au umebadilika tu? Je unaathiri vipi maendeleo ya Afrika? Nini kifanyike kuukomesha?Kupata mengi ungana na mwanahabari wetu Ruben Lukumbuka

  • Maoni ya Wasikilizaji kuhusu habari zetu juma hili ikiwemo hali mashariki mwa DRC

    12/12/2025 Duration: 10min

    Ilivyo desturi ya kila siku ya Ijumaa, ni mada huru. Tunampa msikilizaji wetu nafasi ya kuzungumzia taarifa ambazo tumeziangazia katika habari zetu juma hili, lakini pia matukio mbalimbali nchini mwake.

  • Waasi wa AFC/M23 wanaosaidiwa na Rwanda waudhibiti mji wa Uvira nchini DRC

    11/12/2025 Duration: 09min

    Waasi wa AFC/M23 wanaosaidiwa na Rwanda, ni rasmi sasa wanaudhibiti mji wa kimkakati wa Uvira jimboni Kivu Kusini, hatua inayokuja licha ya wiki iliyopita DRC na Rwanda kutia saini mkataba wa amani.Tunamuuliza msikilizaji anazungumziaje kilichofanywa na waasi wa M23,,Nini kifanyike? na Je, msikilizaji yuko Uvira au amekimbia kutoka Uvira

  • Leo ni siku ya kuadhimisha haki za binadamu duniani lakini ukiukaji waripotiwa

    10/12/2025 Duration: 09min

    Leo ni siku ya kimataifa ya haki za binadamu, hata hivyo dunia inaadhimisha siku hii huku vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vikiendelea kuongezeka kwenye maeneo mbalimbali duniani, maeneo yenye mizozo vitendo hivi vikiwa vya kuogopesha.Tumekuuliza unafikiri kwanini vitendo hivi vinaongezeka licha ya sheria za kimataifa kuwepo?Hali ya haki za binadamu ikoje nchini mwako na Nini kifanyike kuimarisha haki za binadamu ulimwenguni?

  • Upinzani barani Afrika waendelea kunyanyaswa na polisi wakati wa kampeni

    09/12/2025 Duration: 10min

    Mada ya leo ni kuhusu kinara wa upinzani  nchini Uganda Bob Wine pamoja na baadhi ya wagombea wengine wa upinzani wameendelea kunyanyaswa na vyombo vya usalama wanapoendelea na kampeni zao, tume ya uchaguzi ikilaani vitendo hivyo.Yanayofanyika Uganda yanashuhudiwa pia kwenye mataifa kadhaa ya Afrika .Tumemuuliza msikilizaji  Hatua hii ya vyombo vya usalama inaathiri vipi demokrasia na nini kifanyike kujenga mazingira sawa ..Karibu

  • Vita vyashuhudiwa DRC licha ya makubaliano ya kustisha vita kufanyika

    08/12/2025 Duration: 09min

    Licha ya viongozi wa DRC na Rwanda kutia saini mkataba wa amani juma lililopita, mapigano yameripotiwa mashariki mwa Congo kati ya waasi wa M23 na jeshi la Serikali FARDC.Tulimuuliza mskilizaji Je hii ni ishara kuwa mkataba waliotia saini haujazaa matunda ,nani wakuwajibishwa kwa kinachotokea na  Nini kifanywe kuleta utulivu mashariki mwa Congo,,

  • Maoni ya waskilizaji kuhsu taarifa zetu juma hili.

    05/12/2025 Duration: 10min

    Kila ijumaa rfi inakupa nafasi kuchangia mada yoyote kupitia makala ya Habari Rafiki. Skiza kilichopewa kipao mbele kwenye makala ya juma hili.

  • DRC/ Rwanda : Marais wasaini awamu ya mwisho ya mkataba

    05/12/2025 Duration: 10min

    Shaba ya makala haya inalenga nchini DRC, viongozi wa DRC    marais Paul Kagame na  mwenzake Felix Tshisekedi wamesaini, awamu ya mwisho ya mkataba wa amani. Tumekuuliza Je, unadhani wananchi wa mashariki mwa DRC watanufaika moja kwa moja na makubaliano ya worshington?

  • EAC : Wanasiasa wanatumia wahuni kujihami

    03/12/2025 Duration: 10min

    Katika makala haya tujadili hatua ya ongezeko la visa vya wanasiasa wa upande wa serikali na upinzani kutumia makundi ya vijana au wahuni kutisha na kuvuruga mikutano ya mahasimu wao wa kisiasa hili likifanyika hata  kwenye mitandao. Tunakuliza unafikiri kwa nini wanasiasa wanaendelea kutumia makundi ya vijana au wahuni katika siasa. skiza makala haya.

  • Uganda: Je midahalo ina manufaa kuelekea uchaguzi

    02/12/2025 Duration: 09min

    Nchini Uganda, wawaniaji wa urais wameshiriki mdahalo kuelekea uchaguzi wa mwezi ujao, huku rais Museveni akisusia mdahalo huo. Je, unafikiri midahalo huwa na mchango wowote kwa wapiga kura kuelekea siku ya uchaguzi? Skiza baadhi ya maoni ya waskilizaji.

  • Siku ya kimataifa ya kupambana na virusi vya ukimwi

    01/12/2025 Duration: 09min

    Siku ya kimataifa ya mapambano dhidi ya UKIMWI, Umoja wa Mataifa unasema kupungua kwa misaada kunatishia dunia kufikia lengo la kudhibiti ugonjwa huu ifikapo mwaka 2030, huduma za kinga zimevurugika hasa kwenye nchi masikini.  unazungumziaje siku hii, je dunia tumepiga hatua kukabiliana na ugonjwa huu? Skiza maoni ya baadhi ya waskilizaji.

  • Viongozi wa umoja wa ulaya na umoja wa Afrika wakutana Luanda Angola

    26/11/2025 Duration: 10min

    Viongozi wa Afrika na wale wa umoja wa Ulaya wamekutana nchini Angola, lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano wa usalama na kiuchumi, rasilimali za bara hilo zikimulikwa na mataifa yenye nguvu ambayo yameongeza kasi ya uwekezaji kwenye bara hilo. Tumekuuliza unaamini ushirikiano uliopo unanufaisha pande zote ? Ushirikiano wa aina gani Afrika inapaswa kuwa nao na nchi za magharibi?

  • Vitendo vya utekaji kuongezeka Nigeria na baadhi ya nchi za Afrika ya kati

    24/11/2025 Duration: 10min

    Msikilizaji juma lililopita watu wenye silaha waliwateka wanafunzi zaidi ya 300 pamoja na waalimu katika shule moja kwenye jimbo la Niger nchini Nigeria, tukio linalojiri siku chache tangu kutekwa kwa wanafunzi wengine 25 katika shule ya wasichana kwenye jimbo la Kebbi pia huko Nigeria. Vitendo vya utekaji wa watoto vinazidi kuongezeka katika nchi za Afrika magharibi na kati. Nini kifanyike kukomesha vitendo hivyo Afrika?Je taifa lako linashuhudia utekaji wa watoto? Ungana na Ruben Lukumbuka

  • Maoni ya mskilizaji kuhusu matangazo yetu

    23/11/2025 Duration: 10min

    Kila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi ya kuchangi mada yoyote kuhusu taarifa na vipindi vyetu au kile kinafanyika hapo ulipo. Skiza maoni ya waskilizaji juma hili.

page 1 from 2