Synopsis
Listen to interviews, features and community stories from the SBS Radio Swahili program, including news from Australia and around the world. - Sikiza mahojiano, makala na hadithi za jumuiya kutoka Idhaa ya Kiswahili ya SBS Radio, ikijumuisha taarifa za habari kutoka Australia na ulimwenguni.
Episodes
-
#100 More or less? Talking about quantities - #100 Kiasi na idadi
23/01/2026 Duration: 08minLearn how to talk about amounts and quantities in everyday English. - Je, unajua jinsi ya kutumia kiasi na idadi katika kiingereza ya kila siku?
-
Taarifa ya habari:Wanachama wa National wajiuzulu kufuatia sheria tata za hotuba za chuki
23/01/2026 Duration: 11min**Polisi wamsaka mtuhumiwa wa mauaji New South Wales ** Waustralia hamsini na tatu wataiwakilisha taifa kwenye Michezo ya Olimpiki **Na tamasha ya muziki ya Tamworth yaanza kesho.
-
Makala:Serikali ya Victoria kuendelea na ubomozi wa nyumba za umma licha ya upinzani
23/01/2026 Duration: 13minKatika wakati wa mgogoro wa makazi na gharama za maisha, serikali ya Victoria iko katika mchakato wa kubomoa minara yote 44 ya makazi ya umma ya Melbourne. Licha ya upinzani mkubwa na uchunguzi wa bunge unaotaka kusitishwa kwa haraka kwa kazi hizo, serikali ya Victoria inaendelea na mipango hiyo. Kuhama nyumba huchukuliwa kuwa moja ya matukio yenye msongo mkubwa zaidi katika maisha ya mtu. Kwa hivyo, mwaka 2023, wakati maelfu ya wakaazi wa Victoria walipokea taarifa kwamba nyumba zao zitabomolewa wakati fulani kati ya mwaka huo na 2051, msongo ulikuwa dhahiri. Tembelea tovuti yetu sbs.com.au kwa taarifa ama maelezo zaidi.
-
Yaliyojiri Afrika:Mkuu wa jeshi la Uganda atishia kumuua kiongozi wa upinzani Boby Wine
23/01/2026 Duration: 08minKwa maelezo zaidi tembelea tovuti yetu sbs.com.au/swahili.
-
Taarifa ya habari:Nchi za Ulaya zajiandaa kutetea eneo la Denmark
20/01/2026 Duration: 12min**Papa waendelea kuwashambulia watu huko Sydney ** Rais Donald Trump aendelea na mchakato wake wa kuchukua Greenland **Soko la Samaki la Sydney sasa limefunguliwa
-
Makala leo:Mkakati mpya wa usalama wa maji wazinduliwa
19/01/2026 Duration: 07minTangu kuanza kwa kiangazi, watu 33 wamepoteza maisha yao kutokana na kuzama maji huko Australia. Kwa kuwa kuzama maji kunatokea zaidi tangu Janga la COVID-19, Baraza la Usalama wa Maji la Australia limetoa Mkakati Mpya wa Usalama wa Maji wa Australia 2030, ambao unalenga kuimarisha juhudi za kitaifa kupunguza vifo vya kuzama maji kwa asilimia 50 kufikia mwisho wa muongo huu.
-
Yaliyojiri Afrika:Upinzani wakataa matokeo ya uchaguzi Uganda
19/01/2026 Duration: 08minMwanahabari Jason Nyakundi anatujuza yanayoendelea Afrika. Kwa habari ama maelezo zaidi tembelea tovuti yetu sbs.com.au/swahili.
-
Makala leo:jinsi ya kutambua na kuepuka ulaghai wa AI
16/01/2026 Duration: 10minUtafiti mpya unaonyesha kwamba Waustralia wanaamini kupita kiasi juu ya uwezo wao wa kutambua ulaghai wa AI deepfake, hata teknolojia inavyoendelea kuwa ngumu zaidi kugundua. Wataalamu wanatahadharisha kwamba wadanganyifu wanaiba imani na hisia, na wanatoa wito kwa nyinyi kusimama, kuthibitisha na kukataa ujumbe unaotia shaka. Ikiwa mnadhani mngeweza kutambua ulaghai wa deepfake za AI papo hapo, hamko peke yenu. Lakini utafiti mpya wa CommBank unapendekeza kuwa Waustralia wanaweza kuwa na ujasiri zaidi kuliko walivyo sahihi, na matapeli wanastawi katika pengo hilo. Kwa sababu kwa deepfakes, hatari si tu teknolojia. Ni kile inachochukua - uaminifu. Katika Benki ya Commonwealth, Meneja Mkuu wa Huduma za Usimamizi wa Ulaghai wa Kikundi, James Roberts, anasema deepfakes sasa zinatumika kuiga aina za watu tunaozoea kuwaamini, iwe ni mtu maarufu, mtu tunayemfahamu, au mtu tunayempenda.
-
Yaliyojiri Afrika:kura zimeanza kuhesabiwa Uganda licha ya matatizo ya kiufundi hapo awali
16/01/2026 Duration: 09minKwa maelezo au habari zaidi tembelea tovuti yetu sbs.com.su/swahili.
-
Taarifa ya habari:tume ya kifalme ya kuchunguza hotuba za chuki yakosa uungwaji mkono
16/01/2026 Duration: 09min** Kikundi cha Kiyahudi kinatoa wito wa mabadiliko na ucheleweshaji wa marekebisho ya hotuba za chuki za serikali... ** Angalau watu watano wameuawa katika mashambulio ya anga ya Israeli katika Ukanda wa Gaza ** Donald Trump ametishia kutuma wanajeshi kwenda Minneapolis ili kutuliza maandamano yanayoendelea juu ya matendo ya maafisa wa uhamiaji wa shirikisho katika Minnesota.
-
Taarifa ya habari:Kevin Rudd ajiuzulu kama balozi wa Australia nchini Marekani
13/01/2026 Duration: 09min**Kevin Rudd ajiuzulu kama balozi wa Marekani... **Mlipo wa bomu waua maafisa wa polisi kaskazini mwa Pakistan... **Meta yazua shauku kuhusu Australia kuongeza umri wa kutumia mitandao ya kijamii. Kwa habari ama maelezo zaidi tembelea tovuti yetu sbs.com.au/swahili.
-
Yaliyojiri Afrika:Uganda yajiandaa kwa uchaguzi mkuu Alhamisi
12/01/2026 Duration: 09minMwanahabari Jason Nyakundi anatujuza yanayoendelea Afrika. Tembelea tovuti yetu sbs.com.au/swahili kwa maelezo au habari zaidi.
-
Makala leo:utafiti unaonyesha miti kote Australia inakufa kwa kasi zaidi,hali inayochangia kaboni
12/01/2026 Duration: 05minUtafiti mpya umebaini kuwa miti kote Australia inakufa kwa kasi zaidi kuliko inavyokua, hali ambayo inachangia ongezeko la utoaji wa kaboni. Utafiti huo, unaoongozwa na Chuo Kikuu cha Western Sydney na kuchapishwa katika jarida la Nature Plants, umebaini kuwa miti katika aina zote za mifumo ya mazingira - kuanzia misitu ya mvua ya tropiki hadi misitu ya eucalypt - inapungua hali ya hewa inavyozidi kuwa ya joto.
-
Makala leo:Je,uangalizi wa ndege ni jambo maarufu miongoni mwa vijana sasa hivi?
12/01/2026 Duration: 06minMnapofikiria kutazama ndege, labda mnawazia wastaafu. Lakini kizazi kipya kinaanza kutumia darubini na kujihusisha na burudani hii. Kile kilichokuwa kimbilio kutoka ulimwengu wa mtandaoni sasa kinafufuka tena mtandaoni.
-
Taarifa ya habari:Tume ya kifalme yazinduliwa kuchunguza chuki dhidi ya wayahudi
09/01/2026 Duration: 09min**WAZIRI MKUU ANTONY ALBANESE AZINDUA TUME YA KIFALME YA KUCHUNGUZA TUME YA KIFALME YA KUCHUNGUZA KESI ZA CHUKI DHIDI YA WAYAHUDI AUSTRALIA. **MAWIO YA MOTO YAWEKWA SEHEMU MBALIMBALI AUSTRALIA HUKU JOTO IKIZIDI KUONGEZEKA ** KIFO CHA MWANAMKE MAREKANI YAZUA UTATA.
-
Yaliyojiri Afrika:kapteni Ibrahim Traore anusurika jaribio jingine la mapinduzi
08/01/2026 Duration: 09minKwa habari au maelezo zaidi tembelea sbs.com.au/swahili.
-
Afya:wataalamu waonya dhidi ya madhara ya kuchanganya mipango mbalimbali ya lishe
08/01/2026 Duration: 09minMipango ya lishe kama vile Foodmap, yenye protini nyingi, isiyo na gluten, yenye mafuta kidogo, na kula chakula safi - kuna mipango mingi sana ya lishe, na ushauri unaokinzana. Wataalamu wa Australia wanaonya kwamba kufuata mipango mbalimbali ya lishe kwa wakati mmoja kunaweza kuwa na matokeo yasiyotarajiwa.
-
Makala leo:wazazi wapata afueni baada ya serikali kupunguza gharama za vituo vya malezi ya watoto
08/01/2026 Duration: 05minWazazi wanaopeleka watoto kwenye vituo vya malezi wana uhakika wa kupata ruzuku ya asilimia 90 kwa siku tatu za wiki, bila kupitia mchakato wowote wa uthibitishaji. Ruzuku hii itagharimu karibu dola milioni 430 kwa kipindi cha miaka minne ijayo, lakini serikali inasema mamia ya maelfu ya familia zitafaidika.
-
Taarifa ya habari:Maduro na mkewe wakanusha mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya na silaha jijini New York
06/01/2026 Duration: 12min** Rais wa Venezuela Nicolas Maduro na mkewe walikana hatia katika mahakama ya Marekani. ** Mtu anayedaiwa kuwa mfyatuliwa wa risasi Bondi amehamishwa kwenda gereza la Goulbourn supermax. **Na Denmark yaendelea kuikashaifu Marekani kuhusu manoni yao ya Greenland.
-
Yaliyojiri Afrika:Ushahidi mpya waonyesha kuwepo kwa jeshi la Rwanda DRC
05/01/2026 Duration: 08minJason anatujuza yanayojiri pande mbali mbali Afrika, Kwa habari zaidi elekea kwa tovuti yetu sbs.com.au/swahili.