Synopsis
Listen to interviews, features and community stories from the SBS Radio Swahili program, including news from Australia and around the world. - Sikiza mahojiano, makala na hadithi za jumuiya kutoka Idhaa ya Kiswahili ya SBS Radio, ikijumuisha taarifa za habari kutoka Australia na ulimwenguni.
Episodes
-
Taarifa ya Habari: Onyo za mafuriko zawekwa kote jimboni Queensland
06/03/2026 Duration: 14minOnyo za mafuriko zimewekwa kote jimboni Queensland, wakati hali ya hewa ya kitropiki inatabiriwa kufika pwani mchana wa leo kati ya miji ya Cairns na Townsville.
-
Australia Yafafanuliwa: Jinsi makazi ya umma na ya kijamii yanavyo tumiwa nchini Australia
06/03/2026 Duration: 14minKupata mahali pa kuishi pazuri na pa bei nafuu kunazidi kuwa vigumu kwa watu wengi kote Australia.
-
SBS Learn Eng Ep104 Jinsi yakuzungumza kuhusu mitihani
06/03/2026 Duration: 11minJe, unajua jinsi yakuzungumza kuhusu mitihani?
-
Taarifa ya Habari: DFAT yatuma timu kuwasaidia Waaustralia waliokwama Mashariki ya Kati
05/03/2026 Duration: 05minWaziri wa Mambo ya Nje wa Australia Penny Wong amesema dunia ina wasiwasi kuhusu jinsi Iran inavyo jibu mashambulizi ya Marekani na Israel yaliyomuua kiongozi wake, Ayatollah Khamenei na kulenga miundombinu ya nyuklia.
-
Jay "Marekani iki kuambia wanataka mfanye mazungumzo jua nyuma ya pazia wanapanga kitu fulani"
03/03/2026 Duration: 09minSiku kadhaa baada ya Israel na Marekani kuanza mashambulizi yao dhidi ya Iran, wachambuzi wame anza kuelezea madhara ya vita hivyo katika kanda hiyo na duniani kote kwa ujumla.
-
Taarifa ya Habari: Australia haishiriki katika vita dhidi ya Iran, Waziri wa Ulinzi aeleza vyombo vya habari
03/03/2026 Duration: 13minWaziri wa Ulinzi Richard Marles amethibitisha kwamba Australia haishiriki katika hatua za kijeshi zinazoendelea dhidi ya Iran.
-
Yaliyojiri Afrika: Muungano wa Afrika walaani vita dhidi ya iran, waomba vistishwe maramoja
03/03/2026 Duration: 08minViongozi kadhaa wa bara la Afrika wameungana na Muungano wa Afrika kulaani vita vinavyo endelezwa na Marekani na Israel dhidi ya Iran.
-
Makala leo: Wairani-Waaustralia waomba demokrasia baada ya mashambulizi ya Marekani na Israeli
03/03/2026 Duration: 11minWairani-Waaustralia wanaelezea hisia mseto kuhusu mashambulizi ya Marekani na Israel nchini Iran, pamoja na mauaji ya Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei.
-
Taarifa ya habari: Kiongozi mpya wa Iran kuteuliwa baada ya Ayatollah Ali Khamenei kuuawa
02/03/2026 Duration: 05minMchakato unaendelea kuamua ni nani atakaye iongoza Iran, baada ya kuuawa kwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo, Ayatollah Ali Khamenei.
-
Yaliyo jiri Afrika: Tahadhari yatolewa kwa mlipuko wa virusi vinavyo sababisha UVIKO-19 Tanzania
27/02/2026 Duration: 08minWizara ya afya Tanzania imesema kuwa maambukizi ya wagonjwa wa mafua makali ya Influenza na Uviko-19 yameongezeka na kuwataka wananchi kuchukua hatua stahiki za kujikinga na maambukizi hayo.
-
Makala leo: 'Punguza uchochezi' Waziri Mkuu asema baada ya ongezeko ya vitisho dhidi ya wabunge
27/02/2026 Duration: 09minKuondolewa kwa dharura kwa Waziri Mkuu kutoka nyumbani kwake mjini Canberra kwa sababu ya tisho la bomu lililolengwa, kumesababisha maonyo ya kuongezeka kwa mazingira ya usalama, ambapo uadui mtandaoni unazidi kujitokeza kama vitisho vya kimwili vyenye madhara makubwa.
-
Taarifa ya Habari: SES NSW yapokea simu 450 zakuomba msaada wakati wa mafuriko magharibi mwa Sydney
27/02/2026 Duration: 14minMvua kubwa imesababisha mafuriko ya ghafla katika sehemu za Sydney usiku kucha wa Alhamisi hadi Ijumaa, wafanyakazi wakujitolea wa S-E-S wakitoa huduma za uokoaji 44 za maji ya haraka.
-
SBS Learn Eng Ep 102 Jinsi yakuzungumza kuhusu kujipanga
27/02/2026 Duration: 11minJe, unajua jinsi yakuzungumza kuhusu kuchumbiana mtandaoni?
-
Makala leo: Tovuti mpya na App ya kuwalinda wanafunzi wa kimataifa nchini Australia
27/02/2026 Duration: 09minKwa wanafunzi wa kimataifa wanaosomea nchini Australia, kupata huduma ya afya mara nyingi huonekana kama swala ghali sana... au la kutatanisha sana kuweza kuipitia.
-
Taarifa ya Habari: Serikali yaamuru familia za wafanyakazi wa ubalozi nchini Israel na Lebanon kuondoka
26/02/2026 Duration: 07minPolisi wanaamini kuna watu wengi zaidi wanaohusika, katika utekaji nyara na mauaji ya babu mmoja wa Sydney Chris Baghsarian.
-
Yaliyo jiri Afrika: Sudan yaikosoa Uganda kwa kumkaribisha mkuu wa RSF Daglo
25/02/2026 Duration: 09minSerikali ya Sudan inayoungwa mkono na jeshi imekosoa UIganda kwa kumkaribisha mkuu wa wanamgambo wa RSF Mohamed Hamdan Daglo maarufu kama Hemeti.
-
Australia Yafafanuliwa: Zaidi ya mtindo: Jinsi mitindo ya Mataifa ya Kwanza inavyokua nchini Australia
24/02/2026 Duration: 12minKama ume ishi kwa muda wowote nchini Australia, labda umegundua jinsi maisha yalivyo na utulivu.
-
Makala leo: Ubaguzi wa rangi wabainika kuwa umeenea na niwa kimfumo katika vyuo vikuu vya Australia
24/02/2026 Duration: 18minRipoti ya kwanza ya kitaifa kuhusu ubaguzi wa rangi katika vyuo vikuu nchini Australia imegundua kuwa ni tatizo lililo enea na la kimfumo.
-
How to recover from bushfires - Australia Yafafanuliwa: Jinsi yakupona kutokana na moto wa vichaka
24/02/2026 Duration: 10minAustralia’s hot, dry climate and unique landscapes make it one of the most bushfire-prone countries in the world. As climate change drives higher temperatures and drier conditions, we can expect more frequent and more intense bushfires in the future. But once the fire is out, how do you return home safely, find support, and look after yourself? - Hali ya mazingira ya joto, ukavu pamoja na mandhari yakipekee, hufanya Australia iwe mojawapo ya nchi zinazo kabiliwa na moto wa vichaka zaidi dunini. Mabadiliko ya tabianchi yanapo sababisha ongezeko ya hali ya joto na mazingira ya ukame, tunaweza tarajia moto ya vichaka mikali zaidi mara kwa mara katika siku za usoni. Ila moto unapo zimwa, unaweza rudi nyumbani salama, pata msaada na kujihudumia?
-
Taarifa ya Habari: Hali mbaya ya hewa yaweka sehemu nyingi nchini katika hali ya tahadhari
24/02/2026 Duration: 14minSehemu nyingi za Australia ziko katika hali ya juu ya tahadhari, hali mbaya ya hewa na mvua zikiendelea kuathiri jamii na kuharibu njia muhimu za usafiri.