Synopsis
Listen to interviews, features and community stories from the SBS Radio Swahili program, including news from Australia and around the world. - Sikiza mahojiano, makala na hadithi za jumuiya kutoka Idhaa ya Kiswahili ya SBS Radio, ikijumuisha taarifa za habari kutoka Australia na ulimwenguni.
Episodes
-
Yaliyo jiri Afrika: Wakenya waanza kuwatafuta jamaa wao walio ajiriwa na jeshi la Urusi
21/02/2026 Duration: 08minTakriban idadi yawa Kenya 1,000 wameajiriwa kupigania Urusi, kulingana na ripoti ya ujasusi ya Kenya inayoelezea mtandao wa maafisa wahalifu wanaodaiwa kushirikiana na makundi ya biashara haramu ya binadamu.
-
Makala leo: Wito wa mabadiliko makubwa watolewa baada ya wagonjwa wa afya ya akili kutoroka Sydney
21/02/2026 Duration: 11minSerikali ya New South Wales inachunguza mazingira yaliyozunguka kutoroka kwa wagonjwa wawili kutoka hospitali moja, ambao siku chache baadaye walidaiwa kuhusika katika matukio tofauti ambapo watu watatu walifariki.
-
Makala leo: Waumini wa dini laki Islamu wa anza mfungo wa Ramadan nchini Australia na duniani kote
20/02/2026 Duration: 07minMwezi mtukufu wa Ramadan ume anza, Waislamu kote duniani wakisherehekea Iftar katika siku ya pili ya kipindi cha mfungo.
-
Taarifa ya Habari: Polisi wamkamata kakake Mfalme Charles
20/02/2026 Duration: 11minAndrew Mountbatten-Windsor ameachiliwa huru chini ya uchunguzi baada ya polisi wa Uingereza kumhoji kwa saa muda wa masaa 12 kwa tuhuma za utovu wa nidhamu katika ofisi ya umma.
-
SBS Learn Eng Ep 65 Jinsi yakuzungumza kuhusu michezo ya Olimpiki
20/02/2026 Duration: 12minJe, unajua jinsi yakuzungumza kuhusu kuchumbiana mtandaoni?
-
Taarifa ya Habari: Jamii yawa Islamu nchini katika hali ya tahadhari kubwa
19/02/2026 Duration: 05minRipoti mpya ya kiuchumi inaonya Australia ina elekea kupoteza hadhi yake, kama taifa lenye deni la chini, huku mikopo ya serikali ikifikia viwango ambavyo havija onekana tangu vita vya pili vya dunia.
-
SBS Learn Eng Ep 103 Namna yakuzungumza kuhusu kuchumbiana mtandaoni
18/02/2026 Duration: 11minJe, unajua jinsi yakuzungumza kuhusu kuchumbiana mtandaoni?
-
Angus Taylor ashinda kura ya uongozi wa upinzani wa shirikisho
17/02/2026 Duration: 15minAngus Taylor amechukua uongozi wa chama cha Liberal katika kura ya maamuzi ya chama chake kwa ushindi thabiti wa kura 34 dhidi ya 17 zilizotolewa kwa aliyekuwa kiongozi wake.
-
Taarifa ya Habari: Sera ya upinzani yakupiga maarufuku baadhi ya wahamiaji kuingia nchini yazua gumzo
17/02/2026 Duration: 14minMbunge wa chama cha One Nation Barnaby Joyce, amesema ni wazi sera ya uhamiaji ya chama chake, ina ungwa mkono na chama cha Liberal, akihoji madai ya baadhi yama seneta wa chama cha Liberal kuwa hawana taarifa kuhusu mpango huo wa uhamiaji.
-
Yaliyojiri Afrika: Burundi yapewa nafasi ya uwenyekiti AU
17/02/2026 Duration: 08minKuteuliwa kwa Burundi kuwa mwenyekiti wa umoja wa Afrika, kunatarajiwa kuleta tija katika juhudi zakutatuwa migogoro inayo zikabili baadhi ya nchi za jumuia hiyo kutokana na Burundi kuwa na uzoefu katika maswala ya kusimamia amani.
-
ACCC yadai Coles ilidai ilipunguza bei- lakini haikufanya hivyo
17/02/2026 Duration: 07minShirika la uangalizi la watumiaji la Australia, lina fungulia mashtaka duka la Coles katika mahakama ya shirikisho.
-
Taarifa ya Habari: Mshtakiwa wa mauaji ya Bondi afikishwa mahakamani
16/02/2026 Duration: 05minMwanaume ambaye ame shtumiwa kwa kushiriki katika shambulizi laki gaidi katika fukwe ya Bondi, amefikishwa mahakamani.
-
Yaliyojiri Afrika: Upinzani dhidi ya kampuni za USA kupata madini ya DRC waongezeka
13/02/2026 Duration: 09minUpinzani dhidi ya mpango waku ruhusu kampuni za Marekani kupata madini muhimu nchini Jamhuri yakidemokrasia ya Congo, una ongezeka baada ya Rais Tshisekedi kurejea nchini kutoka mkutano wa madini ulio fanyika Marekani wiki iliyopita.
-
Taarifa ya Habari: Sussan Ley astaafu kutoka siasa
13/02/2026 Duration: 14minKiongozi wa upinzani wa kwanza wa kike nchini Australia Sussan Ley ametangaza kuwa amestaafu kutoka siasa.
-
Australia yafafanuliwa: Jinsi yakupona kutokana na moto wa vichaka
13/02/2026 Duration: 15minHali ya mazingira ya joto na ukavu pamoja na mandhari yakipekee, hufanya Australia iwe mojawapo ya nchi zinazo kabiliwa na moto wa vichaka zaidi duniani.
-
Taarifa ya habari:Ziara ya rais wa Israel Isaac Herzog, yazua utata
10/02/2026 Duration: 12min**ZIARA YA RAISI WA ISRAEL AUSTRALIA YAZUA UTATA HUKU WAANDAMANAJI NA POLISI WAKIKABILIANA KATIKA MAANDAMANO DHIDI YA RAIS HUYO ** SERIKALI YAZINDUA MPANGO WA KWANZA WA FAMILIA NA UNYANYASAJI WA WANAWAKE NA WATOTO WA MATAIFA YA KWANZA. **NA CHAMA CHA LIBERAL BADO LIANENDELEA KUWA NA MZOZO WA UONGOZI WA CHAMA BAADA YA KUGAWANYIKA KWA SIKU 17
-
Yaliyojiri Afrika:Rwanda haikubali kutishwa na Marekani
10/02/2026 Duration: 07minKwa habari na melezo zaidi, tembelea tovuti ya sbs.com.au.
-
What actually happened on January 26? - Australia yafafanuliwa:Nini kilifanyika Januari 26?
10/02/2026 Duration: 08minJanuary 26 is one of the most debated dates in Australia’s history. Often described as the nation’s birthday, the day marks neither the formal founding of the colony nor the creation of the Commonwealth. Instead, it reflects a layered history shaped by colonisation, political decisions, and ongoing First Nations resistance. Understanding what actually happened on January 26 reveals why the date is experienced so differently across the country. - Tarehe 26 Januari ni moja ya tarehe zinazojadiliwa sana katika historia ya Australia. Mara nyingi inatajwa kama siku ya kuzaliwa ya taifa, lakini siku hiyo haimaanishi kuundwa rasmi kwa koloni au kuanzishwa kwa Jumuia. Badala yake, inaakisi historia yenye tabaka nyingi inayoundwa na ukoloni, maamuzi ya kisiasa, na upinzani unaoendelea wa Mataifa ya Kwanza. Kuelewa kilichotokea hasa tarehe 26 Januari kinafunua ni kwa nini tarehe hiyo inaathiriwa kwa namna tofauti katika nchi nzima.
-
Makala leo:Australia na Indonesia wasaini mkataba wa usalama
09/02/2026 Duration: 08minWaziri Mkuu Anthony Albanese amepongeza makubaliano mapya ya usalama na Indonesia kama mabadiliko muhimu kuelekea ushirikiano wa karibu wa ulinzi kati ya nchi hizi mbili. Hata hivyo, wachambuzi wanaonya kwamba mkataba huo unaweza kuja na gharama kubwa, ikiwezekana kupuuza masuala ya haki za binadamu yanayoendelea huko Papua Magharibi na wasiwasi kuhusu mwelekeo wa kisiasa wa siku zijazo wa serikali ya Indonesia
-
Makala leo:Shirika la Haki za Binadamu laonya kuwa demokrasia iko hatarini ikilinganishwa na miaka ya 1980
09/02/2026 Duration: 10minDemokrasia na utaratibu wa kimataifa unaozingatia sheria ziko hatarini, kulingana na ripoti ya kila mwaka ya Shirika la haki za binadamu ama Human Rights Watch. Kuna msisitizo mahususi juu ya Marekani na kile ambacho chombo cha kimataifa kinaelezea kama kudorora kwa haki za binadamu, lakini pia kuna tahadhari juu ya Australia. Sera za uhamiaji na kuwekwa kizuizini kwa vijana za Australia zinaorodheshwa kama 'mapungufu makubwa', zikionyeshwa kuwa ni demokrasia pekee ya Magharibi isiyo na sheria ya kitaifa ya haki za binadamu.