Jua Haki Zako

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 3:56:45
  • More information

Informações:

Synopsis

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.

Episodes

  • Kenya : Ahadi ya serikali kwa jamii za wachache

    23/12/2025 Duration: 09min

    Kila disemba 18 dunia huadimisha siku ya  Kimataifa ya Jamii za Walio Wachache  siku inayolenga kuzikumbusha serikali na jamii wajibu wa kulinda haki, heshima na ushirikishi wa makundi ambayo kwa miaka mingi yamekuwa yakidai kuachwa nje mipango ya serikali Nchini Kenya, jamii za walio wachache, zikiwemo jamii za wafugaji wanaohamahama, zimekuwa zikidai hazitambuliwi kikamilifu, kukosa huduma za msingi, na kutengwa katika maamuzi muhimu ya kitaifa. Makala haya yanaangazia mipango ya serikali ya Kenya kwa jamii hizo.

  • Mpango wa kidijitali uliokwama unavyowanyima wanafunzi elimu ya kisasa Kenya

    21/12/2025 Duration: 10min

    Mwaka 2016, Serikali ya Kenya ilizindua Mpango wa Mafunzo kwa Njia ya Kidijitali (DLP), ikiahidi kubadilisha elimu ya msingi ya umma kupitia teknolojia. Awamu ya kwanza ikigharimu walipa kodi zaidi ya Shilingi bilioni 30, huku kukiwa na mpango wa kupanua mradi huo kwa makadirio ya Shilingi bilioni 64. Takribani miaka kumi baadaye, mpango huo unazidi kukabiliwa na matatizo makubwa na hatimaye kukwama hivyo kuwanyima wanafunzi wa shule za msingi haki zao za kupata elimu ya kidijitali.Sikiliza

  • Kenya : Haki ya wafanyakazi nje ya nchi

    19/12/2025 Duration: 09min

    Katika Juhudi za raia wa Africa Kutafuta ajira nje ya nchi wengine wamejipata katika njia panda. Lakini ubalozi wa Austria nchini Kenya, unasisitiza taifa hilo ni salama kwa wafanyakazi wa kigeni. Skiza makala haya.

  • EAC : Haki ya matumizi ya mitandao

    02/12/2025 Duration: 09min

    Je unafahamu haki zako wakati unatumia mitandao? na Je unafahamu kwamba haustahili kuvuka kiwango fulani wakati unatumia mitandao? Paul Brain ni mtaalamu  wa matumizi ya mitandao anafanunua masharti ya matumizi ya mitandao.

  • Kenya: Msimamo wa wavuvi wa Lamu kuhusu mbinu za kuvua samaki

    29/11/2025 Duration: 09min

    Kwa muda sasa wavuvi kutoka kaunti ya Lamu, nchini Kenya, wamekuwa wakizozana na serikali kuhusiana na mbinu za kisasa wa uvuvi kutokana na misimo wa serikali kuwataka watumie technolojia katika uvuvi. Mwaka 2016 serikali ya Kenya ilipitisha sheria ya kuwataka wavuvi kutumia mbinu za kisasa kuendesha shughuli za uvuvi lakini hili limeibua changomoto miongoni mwa wavuvu wanaosisitiza kutumia mbInu za kale kuendesha shughuli za uvuvi kutokana na sababu kadhaa. skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.

  • Kenya : Ukeketaji bado changamato Africa

    20/11/2025 Duration: 09min

    Katika maeneo ya wafugaji wa kuhamahama nchini Kenya, mila na desturi bado zinaonekana kupewa kipaumbele kuliko elimu – hali inayowafanya wasichana kuwa katika hatari kubwa ya kukeketwa.   Wasichana wengi hukatizwa masomo na kulazimishwa kufuata tamaduni zinazokiuka haki zao, huku ukeketaji ukiendelea kufanywa kwa usiri mkubwa licha ya juhudi za serikali na wadau kutoa elimu na kupiga marufuku tendo hilo.   Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa ukeketaji wa wasichana na wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 49 bado ni tatizo linaloripotiwa nchini Kenya. Katika makala haya  tunaangazia namna tamaduni hizi zimeendelea kushamiri katika jamii za wafugaji wa kuhama hama na jinsi zinavyomnyima mtoto wa kike haki yake ya kupata elimu na kuishi bila unyanyasaji.

  • Matumizi ya hadithi kupigania haki

    17/11/2025 Duration: 09min

    Katika makala haya tunangazia safari ya kutetea haki za binadamu kwa kutumia hadithi sauti moja, uzoefu, na ujasiri wa mtu kusimulia alichopitia. Tasisi ya  Moth, imekuwa ikitumia hadithi kama si tu kwa mudhadha wa burudunai bali ni daraja linalounganisha ukweli wa mtu mmoja na uelewa wa dunia nzima.  Hadithi nyingi ni za binafsi, lakini hisia zinazozibeba—hofu, matumaini, maumivu au ushindi—ni za ulimwengu mzima. Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Mila zanakandamiza wanawake nchini Kenya

    17/11/2025 Duration: 09min

    Mila na tamaduni kutoka jamii mbalimbali nchini Kenya,  zimezidi kukandamiza wanawake kutoridhi mali. Pwani ya Kenya, changamoto hiyo pia imeathiri wanawake wajane skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.

  • DRC : Ukatiloia wa jinsia wakithiri

    28/10/2025 Duration: 09min

    Skiza makala haya kufahamu mengi

  • DRC : Haki za raia wanaoishi na ulemavu Goma, DRC

    25/10/2025 Duration: 09min

    Katika makala haya  shaba yetu inalenga nchini DRC hasa eneo la Mashariki, ambapo tunajadili haki za malemavu eneo hilo. Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mamia ya watu wenye ulemavu wamejikuta wakihangaika kuokoa maisha yao, kipindi hiki vita vikiendelea kusheheni eneo hilo. Miji kama Goma, Rutshuru na Sake imeshuhudia maelfu wakikimbia maakazi yao. Lakini kwa wengi wenye ulemavu, kukimbia si jambo rahisi. Wengine wanatembea kwa magongo, wengine hutumia viti vya magurudumu ambavyo haviwezi kuvuka matope, milima, au mabonde. Skiza makala haya kufahamu mengi

  • Uganda : Uchaguzi raia wanafahamu haki zao

    18/10/2025 Duration: 09min

    Uchaguzi nchini Uganda, unatarajiwa kufanyika mwezi  January, Rais Museveni akichuana tena na Hasimu wake wa kisiasa mwanamziki aliyeukia siasa, Bobi Wine. Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Kenya/Nigeria : Wanawake wanahangaishwa kwa mitandao

    06/10/2025 Duration: 10min

    Katika makala haya  tunaangazia suala linalozidi kuwa pasua kichwa—unyanyasaji wa wanawake kwenye mitandao ya kijamii. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na shirikisho la mawakili wanawake nchini Kenya FIDA, kwa ushirkiano na wenzao wa kutoka nchini Nigeria, unaonesha kuwa karibu kila mwanamke anayetumia mitandao amewahi kushambuliwa iwe ni kwa maneno ya matusi, vitisho, au kusambaziwa picha binafsi bila idhini yake. Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.

  • DRC : Unyanyasaji wa haki za watoto

    05/10/2025 Duration: 09min

    Watoto wanatumika kwa baishara ya ngono Skiza makala haya kufahamu mingi zaidi

  • Kenya: Wayu Daba wapokeahati miliki ya shamba

    23/09/2025 Duration: 10min

    Katika makala haya  tunaangazia hatua ya kihistoria kwa jamii ya wafugaji nchini Kenya. Jamii ya Wayu Daba imekabidhiwa rasmi hati miliki ya ardhi yao kupitia Mpango wa Kusimamia Ardhi Kidigitali, unaoendeshwa na serikali  mradi unaotekelezwa kwa ushirikiano na Shirika la Chakula na Kilimo, FAO. Hati hii inaguza maeneo makubwa ya ardhi, ikiwemo ardhi loevu yenye rutuba, misitu ya kiasili yenye wanyama na mimea adimu, pamoja na maliasili zinginezo ambazo zimekuwa nguzo ya maisha ya jamii hiyo kwa vizazi vingi Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Africa : Haki ya waandishi wa vitabu

    19/09/2025 Duration: 10min

    Katika makala haya  tutajadili haki za mwandishi wa vitabu, Je, mwandishi wa kitabu ana haki gani anapochapisha kitabu chake katika mashirika ya uchapishaji? Ni kipi kinafaa kuzingatiwa katika mchakato wa uchapishaji? Maswali haya yote yanamzunguka mwandishi, mchapishaji na shirika la uchapishaji ili kuibuka na mwafaka katika tasnia ya uandishi. Na ndiyo baadhi ya mambo yanayojadiliwa kwenye makala haya.

  • Maandiko matakatifu yapewe nafasi kusuluhisha mizozo

    17/09/2025 Duration: 10min

    Katika makala haya tunaangazia safari ndefu ya amani katika mataifa yanayopitia migogoro, Shabaha ikiwa ni Sudan Kusini na Somalia. Mataifa haya yamepitia miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, mizozo ya kisiasa, na changamoto za kiusalama ambazo zimeathiri mamilioni ya raia wao.  Lakini katikati ya changamoto hizo, mashirika mbalimbali ya kimataifa na ya kikanda yamekuwa mstari wa mbele kusukuma gurudumu la amani. Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Mashambulizi kupitia mitandao ya kijamii

    02/09/2025 Duration: 09min

    Mitandao ya kijamii na teknolojia za kidijitali zimekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Tunawasiliana, tunajifunza, tunafanya biashara na hata kushiriki mijadala ya kitaifa kupitia mitandao. Lakini pamoja na manufaa haya, kumekuwa pia na changamoto kubwa: mashambulizi ya maneno, udukuzi wa akaunti, na hata ulaghai wa kifedha. Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Je mchango wa wanawake ni upi katika juhudi za kupigania haki zao

    29/08/2025 Duration: 09min

    Wanawake wametuhumiwa kwa kukosa kupigania haki zao, lakini msimamo huu unakanusha na wengi. Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Dunia: watoto wanazidi kutumika kama vijakazi

    23/08/2025 Duration: 10min

    Mwezi wa Juni ulishuhudia matukio mawili muhimu ya kimataifa yakiangazia haki na ustawi wa watoto. Mnamo tarehe 12 Juni, dunia iliadhimisha Siku ya kupinga Ajira ya Watoto, (World Day Against Child Labor) ikirejelea takwimu za kutisha kwamba watoto milioni 160 duniani kote bado wamenaswa katika ajira ya watoto - wengi wakifanya kazi chini ya mazingira hatarishi. Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Africa : Mazingira yanavyoathiri haki za watoto

    22/08/2025 Duration: 09min

    Katika makala haya tunangazia uharibifu wa mazingira unavyoathiri haki za  watoto. Skiza makala haya kufahamu zaidi.

page 1 from 2