Synopsis
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.
Episodes
-
Kenya : Haki ya kumiliki ardhi ya jamii ya wafugaji
22/08/2025 Duration: 10minJamii za wafugaji nchini Kenya, bado zinapitia changamoto za kumiliki ardhi, jamii hizo ni kama vile,Turkana, Samburu, Rendille, Borana, Gabra na nyingine , zimeathiriwa kwa muda mrefu na unyang’anyi wa ardhi wakati wa ukoloni, ambao uliendelezwa hata baada ya uhuru . Licha ya kutambuliwa kwa haki za jamii katika Katiba ya 2010 na kupitishwa kwa Sheria ya Ardhi ya Jamii ya mwaka 2016, jamii hizi bado zinakumbwa na changamoto za ardhi,unyang’anyaji wa mashamba na ukosefu wa haki za kisheria—hali inayotishia siyo tu maisha yao bali pia utamaduni.
-
EAC : Uhuru na haki ya wanahabari kujiunga miungano
30/07/2025 Duration: 09minKataika makala haya tunajadili umuhimu wa wanahabari kuelewa na kulinda haki zao, hasa kupitia vyama na miungano ya waandishi wa habari. Katika mazingira ambapo uhuru wa habari uko mashakani, na waandishi wengi wanakumbwa na changamoto kazini, je, kuna msaada wowote wa pamoja? Ni moja tu ya maswali tunayatarajia kuyajibu kwenye makala ya haya. Skiza makala haya kufahamu mengi
-
EAC : Wakimbizi wazidi kukimbia makwao wakitafuta amani
28/07/2025 Duration: 10minMaelfu ya watu kote barani Afrika wanalazimika kuyahama makazi yao—wengine kwa sababu ya vita, wengine kwa sababu ya mateso au hali ngumu ya maisha. Wanakimbilia nchi jirani wakitafuta usalama, hifadhi, na matumaini ya kuanza upya, lakini safari ya kuwa mkimbizi si rahisi, ni safari ya maumivu, vizingiti, na kupoteza mengi. Katika makala haya tunajadili visingiti wanavyokumbana navyo watu wanaokimbia maakazi yao kutokana na vita. Skiza makala haya kufahamu mengi.
-
Kenya : Haki ya mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa
17/07/2025 Duration: 09minkatika makala haya mskilizaji tunazAma kuangazia uamuzi wa kihistoria uliofanywa hivi majuzi na Mahakama ya juu zaidi ya Kenya kuhusu haki za mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ya dini ya Kiislamu—hasa kuhusu haki ya kurithi mali ya baba yake. Uamuzi huu umetangazwa kuwa hatua muhimu katika mapambano ya kuhakikisha kila mtoto anaheshimiwa na kulindwa kikatiba bila kujali dini au mazingira ya kuzaliwa kwake. Kwa miongo mingi, baadhi ya watoto waliozaliwa nje ya ndoa, hasa katika jamii za Kiislamu, wamekuwa wakinyimwa haki ya kurithi mali ya baba zao moja kwa moja kwa mujibu tamaduni ya dini hiyo. Kufamu mengi skiza makala haya.