Habari Za Un

Informações:

Synopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodes

  • Akili Mnemba inarahisisha mambo lakini inahitaji usimamizi - Profesa Pillay

    31/05/2024 Duration: 03min

    Kila uchao, mikutano ifanyika kona mbali mbali za dunia kubonga bongo ni kwa vipi akili mnemba inaweza kutumika kwa manufaa ya binadamu na si vinginevyo kwani Umoja wa Mataifa unataka nyenzo hiyo iwe ya manufaa hasa katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu. Huko Geneva, Uswisi kumetamatika mkutano wa kujadili ni kwa vipi akili mnemba italeta manufaa. Suala hilo hilo pia lilikuwa miongoni mwa mijadala ya jukwaa la 4 la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali huko Manama, Bahrain ambapo mmoja wa wanajopo alikuwa Profesa Dokta Selvaraj Oyyan Pillay kutoka Malaysia ambaye katika makala hii Assumpta Massoi alizungumza naye na kuumuliza iwapo ana shaka na shuku kuhusu mustakabali wa akili mnemba na nini kifanyika.

  • UNICEF inawasaidia wanafunzi wenye ulemavu wa kutosikia kujifunza kidijitali nchini Kenya

    31/05/2024 Duration: 01min

    Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kupitia mradi unofahamika kama GIGA, kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu, wameunganisha wanafunzi zaidi ya 257,000 kwenye mtandao wa Intaneti, wakiwemo wanafunzi 7,690 wenye mahitaji maalum, na pia mafunzo ya kidijitali kwa maelfu ya walimu.Mmoja wa walimu walionufaika na mafunzo hayo ni Terika Gevera, Mwalimu katika Shule ya Viziwi ya Maseno katika Kaunti ya Kisumu."Wanafunzi wetu mara nyingi hupata ujifunzaji wao kupitia hisia ya kuona, kwa sababu usikivu wao hauwafai sana. Kwa hivyo, UNICEF kuunganisha shule kwenye intaneti kumesaidia sana hasa katika kuboresha ufundishaji wetu. Watoto wetu wanaweza kujifunza na hasa kujifunza kupitia njia ya kuona wanaweza kupata maarifa kwa njia bora zaidi.”Mwalimu Terika Gevera anafafanua zaidi akisema,"Intaneti ni sehemu muhimu sana katika kujifunza. Tuliamunganishwa katika nyenzo za E-Kitabu. E-Kitabu wamejaribu kuandika hadithi zao kwa lugha ya ishara, hivyo wanafunzi hutazama picha, huangalia ishar

  • 31 MEI 2024

    31/05/2024 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Burkina Fasso na mradi unofahamika kama GIGA unaosaidia kufanikisha masomo ya kidijitali kwa wanafunzi nchini Kenya. Makala inamulika usimamizi wa Akili Mnemba na mashinani inatupeleka Garissa nchini Kenya, kulikoni?Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo ameelezea wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la hivi karibuni la mauaji ya raia nchini Burkina Faso, huku kukiwa na madai ya kuwajibika na mauaji hayo kutoka pande zote, makundi yenye silaha na serikali. Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kupitia mradi unofahamika kama GIGA, kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu, wameunganisha wanafunzi zaidi ya 257,000 kwenye mtandao wa Intaneti, wakiwemo wanafunzi 7,690 wenye mahitaji maalum, na pia mafunzo ya kidijitali kwa maelfu ya walimu.Makala inaturejesha Bahrain kufuatilia usimamizi wa Akili Mnemba wakati huu ambapo huko Geneva, wabobezi wa Akili Mnemba na wawakilishi kutoka sekta ya umma na binafsi wakib

  • Volker Türk: Mauaji ya raia Burkina Faso yamefurutu ada lazima yakome

    31/05/2024 Duration: 01min

    Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo ameelezea wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la hivi karibuni la mauaji ya raia nchini Burkina Faso, huku kukiwa na madai pande zote, makundi yenye silaha na serikali kuhusika na mauaji hayo. Kwa mujibu wa tarifa ya ofisi ya Kamishina Mkuu wa haki za binadamu OHCHR kati ya Novemba 2023 na Aprili mwaka huu 2024 imepokea madai ya ukiukwaji wa haki na ukatili unaokiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu ukiwaathiri takriban watu 2732 hili likiwa ni ongezeko la asilimia 71 ya visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu ukilinganisha na miezi sita iliyopita.Taarifa inasema watu 1794 ay asilimia 65 miongoni mwa watu hao ni waathirika wa mauaji ya kinyume cha sheria.Ofisi hiyo ya haki za binadamu imesema Makundi yenye silaha, kama vile Jamāʿat nuṣrat al-islām wal-muslimīn, Kundi kubwa la Kiislamu katika Jangwa la Sahara na makundi mengine yanayofanana na hayo, yamezidisha mashambulizi yao dhidi ya raia, ikiwa ni pamoja na dhidi ya wakimb

  • Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno "Kibuhuti"

    30/05/2024 Duration: 56s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili  leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KIBUHUTI” 

  • 30 MEI 2024

    30/05/2024 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika ni kwa vipi wabunifu wanaweza kumiliki kazi zao na zikasongesha SDGs ikiwemo kutokomeza umaskini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za Sudan, Gaza na jukwaa la Kimataifa la “AI for Good”, pamoja na uchambuzi wa neno la wiki.Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa leo yametoa onyo kali kwamba dalili zote zinaonesha kuzorota kwa kiasi kikubwa kwa hali ya lishe kwa watoto na wanawake katika nchi ya Sudan inayokumbwa na vita. Uchambuzi wa hivi karibuni uliofanywa na Mashirika hayo matatu la Kuhudumia Watoto (UNICEF), la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na la afya ulimwenguni (WHO) unaonesha kwamba uhasama unaoendelea unazidisha visababishi vya utapiamlo kwa watoto. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kutoa wito wa usitishaji mapigano katika Ukanda wa Gaza kwasababu hali inazidi kuwa tete kila uchao. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema hakuna mengi ambayo linaweza kufanya kwa sasa huko Rafah kwani akiba ya

  • Nilikuwa na ujauzito wa miezi tisa nyumba yangu ilipopigwa bomu - Simulizi ya mkimbizi Sudan

    29/05/2024 Duration: 02min

    Makala hii inatupeleka nchini Sudan kuangazia maisha ya Sara, mmoja wa wakimbizi wa ndani katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika. Sara alikuwa na ujauzito wa miezi 9 wakati bomu lilipopiga nyumba yake na kumlazimu kukimbia na hatimaye kujifungua mtoto wake peke yake bila uangalizi wowote wa kitabibu. Familia nyingi nchini Sudan zimesambaratishwa na mzozo unaoendelea. Selina Jerobon ndiye msimulizi wetu..

  • 29 MEI 2024

    29/05/2024 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa. Makala inatupeleka nchini Sudan kusikia simulizi ya mmoja wa wakimbizi na mashinani tunakupelekea nchini Ethiopia kusiki jinsi ambavyo wasichana wanavyosaidiwa kubaki shule.Leo ni siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa mwaka huu ikibeba maudhui “Kuwa tayari kwa ajili ya ujenzi wa mustakbali bora kwa pamoja”. Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa ulinzi wa amani unasialia kuwa ushirikiano wa kipekee  wa kimataifa. Mshauri wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kijeshi, Jenerali Birame Diop amesema kadri binadamu wataendelea kuweko duniani mizozo na majanga yataendelea kuweko na hivyo kinachohitajika ni mfumo wa kupunguza uweko na utatuzi wa majanga hayo.Makala inatupeleka nchini Sudan kuangazia maisha ya Sara, mmoja wa wakimbizi wa ndani katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.Na mashinani tutaelekea Gambella nchini Ethiopia  kusikia ni kwa jinsi gani shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto&nbs

  • Ulinzi wa amani wa UN ni ushirikiano wa kipekee wa kimataifa

    29/05/2024 Duration: 02min

    Leo ni siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa mwaka huu ikibeba maudhui “Kuwa tayari kwa ajili ya ujenzi wa mustakbali bora kwa pamoja”. Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa ulinzi wa amani unasialia kuwa ushirikiano wa kipekee  wa kimataifa. Katika ujumbe wake kwa siku hii Antonio Guterres amesema "Leo tunawaenzi walinda amani zaidi ya 76,000 wa Umoja wa Mataifa ambao wanadumisha lengo bora zaidi la ubinadamu, amani. Siku baada ya siku, wakihatarisha Maisha yao, wanawake na wanaume hawa wanafanya kazi kwa ujasiri katika baadhi ya maeneo hatari na yasiyo na utulivu duniani ili kulinda raia, kudumisha haki za binadamu, kumsaidia masuala ya uchaguzi na kuimarisha taasisi. Zaidi ya walinda amani 4,300 wamelipa gharama ya Maisha yao wakati wakihudumu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa. Hatutawasahau kamwe.”Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa maudhui ya siku ya mwaka huu yanaashiria kwamba wakati ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa umethibitika kuwa sehemu ya suluhu kwa zaidi ya miaka 75 uk

  • Jenerali Birame Diop: Ulinzi wa amani uwe na mkakati wa kudhibiti habari potofu na za uongo

    29/05/2024 Duration: 01min

    Mshauri wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kijeshi, Jenerali Birame Diop amesema kadri binadamu wataendelea kuweko duniani mizozo na majanga yataendelea kuweko na hivyo kinachohitajika ni mfumo wa kupunguza uweko na utatuzi wa majanga hayo.Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku ya walinda amani duniani, Jenerali Diop ambaye anatamatisha jukumu lake anasema angalau kwa sasa kuna jawabu la ulinzi wa amani ambalo licha ya changamoto zake linaleta nuru.“Na ulinzi wa amani umethibitisha kuwa unaweza kutatua baadhi ya mizozo. Ninaweza kukupatia mfano wa Timor-Letse [TIMORLETSI]. Ninaweza kukupa mifano ya Côte d'Ivoire, ya Sierra Leone, ya Liberia, ambako ulinzi wa amani umesaidia kurejesha amani na utulivu. Na sasa nchi hizi hata zinashiriki kwenye ulinzi wa amani.”Ingawa ulinzi wa amani unazaa matunda, kwa Jenerali Diop ambaye anatoka Senegal, jambo muhimu ni kuzidi kuboresha huduma hiyo kwani itaendelea kuwa muhimu huku Umoja wa Mataifa ukihakikisha ujumbe wa ulinzi wa amani unapatiwa m

  • 28 MEI 2024

    28/05/2024 Duration: 10min

    Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea-Watu zaidi ya 2000 wahofiwa kufunikwa na maporomoko ya udongo Papua New Guinea , Umoja wa Mataifa wasaidia-Ripoti ya UNRWA inasema wakimbizi wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na dharura ya kiafya isiyokuwa na mfano wake iliyosababishwa na vita mbaya zaidi katika historia ya Gaza- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres  ameuambia Mkutano wa nne wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa Vidogo Zinazoendelea (SIDS4) Antigua na Barbuda kwamba ulimwengu unahitaji kuchukua hatua ili kusaidia vyema na kuhamasisha ufadhili kwa Nchi za Visiwa Vidogo Zinazoendelea (SIDS) -Katika kuelekea siku ya walindamani hapo kesho leo kikosi cha Tanzania TANZBAT11 nchini DRC chashikamana na wananchi katika miradi mbalimbali-Na mashinani utamsikia mlindamani kutoka Italia anayehudumu katika mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL

  • Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ yaamua juu ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu Gaza

    24/05/2024 Duration: 01min

    Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ leo imetoa maamuzi ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari katika Ukanda wa Gaza Flora amefuatilia uamuzi huo.Leo Kwa kura 13 dhidi ya 2 mahaka ya ICJ imeamua kwamba:1. Inathibitisha tena hatua za muda zilizoainishwa katika Maagizo yake ya tarehe 26 Januari 202 na 28 Machi 2024, ambayo yanapaswa kutekelezwa mara moja na kwa ufanisi2. Imeainisha hatua zifuatazo za muda kwamba : Taifa la Israeli, kwa kuzingatia wajibu wake chini ya Mkataba juu ya Kuzuia na Adhabu ya Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari, na kwa kuzingatia hali mbaya ya maisha inayowakabili raia katika Jimbo la RafahIsitishe mara moja mashambulizi yake ya kijeshi, na hatua nyingine yoyote katika jimbo la Rafah ambayo yanaweza kusababishia kundi la Wapalestina Gaza hali hiyo ya maisha inayoweza kuleta uharibifu wa kimwili kwa ujumla au sehemu;Iendeleel kukiacha wazi kivuko cha Rafah  kwa utoaji usiozuiliwa kwa kiwango cha haraka cha hud

  • WHO: COVID-19 imerudisha nyuma muongo wa maendeleo ya umri wa watu kuishi

    24/05/2024 Duration: 02min

    Ripoti mpya ya Takwimu za Afya Ulimwenguni iliyotolewa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, inaonyesha kuwa janga la COVID-19 limebadilisha mwelekeo wa kuongezeka kwa umri wa watu kuishi wakati wa kuzaliwa na matarajio ya maisha yenye afya wakati wa kuzaliwa HALE.Ripoti hiyo ya takwimu za afya ulimwenguni hutolewa kila mwaka na WHO ikijumuisha viashirikia vya afy na vinavyohusiana na imekuwa ikitolewa tangu mwaka 2005.Ripoti yam waka huu kwa mujibu wa WHO imetathimini Zaidi ya viashiria 50 vinavyohusiana na afya kuanzia malengo ya maendeleo endelevu SDGs na mikakati kazi 13 ya WHO au GPW13.Ripoti inasema Janga la COVID-19 limefuta karibu muongo mmoja wa maendeleo katika kuboresha umri wa watu kuishi ndani ya miaka miwili tu. Kati ya 2019 na 2021, umri wa kuishi duniani ulipungua kwa mwaka 1.8 hadi miaka 71.4 ukirejea nyuma hadi kiwango cha mwaka 2012.”Pia ripoti imeongeza kuwa umri wa kuishi kwa afya duniani ulipungua kwa miaka 1.5 hadi miaka 61.9 mwaka 2021 ukiwa umerudi nyuma kwenye kiwan

  • Wanajeshi walinda amani wa UN wana majukumu mengine muhimu zaidi ya bunduki: TANBAT 7

    24/05/2024 Duration: 03min

    Zikiwa zimesalia siku chache kufika Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mei 29, tunaangazia shughuli zao na kuwatia moyo na leo tunaelekea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwasikia baadhi yao kutoka katika  Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR (MINUSCA)

  • FAO na wadau wawakutanisha wadau wa kilimo na chakula Tanzania

    24/05/2024 Duration: 03min

    Nchini Tanzania, kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na wadau wake kama Kitovu cha Kuratibu Mifumo ya Chakula cha Umoja wa Mataifa, Kikundi cha Washirika wa Maendeleo ya Kilimo na Lishe, wakulima, sekta binafsi, na watafiti na Taasisi za kitaaluma wamekutana mjini Morogoro ili kupitia na kuboresha vipaumbele na ramani ya mifumo ya chakula iliyoanzishwa mwaka 2021. Hamad Rashid wa Redio washirika wetu Mviwata FM ya Mkoani Morogoro amehudhuria Kikao hicho na kuandaa taaarifa hii. 

  • 24 MEI 2024

    24/05/2024 Duration: 10min

    Hii leo jaridani tunaangazia maamuzi ya ICJ ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel, na  mifumo ya chakula nchini Tanzania. Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR na mashinani nchini Kenya, kulikoni? Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ leo imetoa maamuzi ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari katika Ukanda wa Gaza Flora amefuatilia uamuzi huo. Nchini Tanzania, kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na wadau wake kama Kitovu cha Kuratibu Mifumo ya Chakula cha Umoja wa Mataifa, Kikundi cha Washirika wa Maendeleo ya Kilimo na Lishe, wakulima, sekta binafsi, na watafiti na Taasisi za kitaaluma wamekutana mjini Morogoro ili kupitia na kuboresha vipaumbele na ramani ya mifumo ya chakula iliyoanzishwa mwaka 2021.Katika makaala zikiwa zimesalia siku chache kufika Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mei 29, tunaangazia shughuli zao na

  • Jifunze Kiswahili: Pata ufafanuzi wa methali “Kanga hazai ugenini.”

    23/05/2024 Duration: 01min

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Kanga hazai ugenini.”

  • 23 MEI 2024

    23/05/2024 Duration: 10min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada ka kina inayotupeleka huko wilaya ya Abyei iliyoko kati ya mpaka wa Sudan Kusini na Sudan lilifanyika shambulizi la kuvizia wakati gari la Umoja wa Mataifa lilipokuwa likisafirisha raia waliojeruhiwa, ambalo lilisababisha kifo cha mlinda amani. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali “Kanga hazai ugenini.”  Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza ugonjwa wa Fistula ambalo ni tundu kati ya njia ya uzazi na kibofu cha mkojo, inayosababishwa mara nyingi na uchungu wa muda mrefu wakati wa kuelekea kujifungua, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na masuala ya kijinsia UNFPA Natalia Kanem amesema Fistula ya uzazi ni matokeo ya kusikitisha ya kushindwa kulinda haki za uzazi za wanawake na wasichana walio katika mazingira magumu zaidi na ni lazima itokomezwe kwa watu wote. Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Palestina Matthew Hollingworth ameandika katika ukurasa wake wa mtanda

  • Waathirika Garisa Kenya washukuru UNICEF kwa msaada wa fedha baada ya mafuriko

    22/05/2024 Duration: 03min

    Kenya inashuhudia kiwango kikubwa cha mvua zaidi ya kile cha kawaida ambacho kimesababisha mafuriko makubwa,maporomoko ya udongo na maelfu ya watu kutawanywa hivi karibuni. Miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi ni Kaunti ya Garisa , ambako hivi sasa asante kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake kama shirika la Norway kwa ajili ya ushirikiano wa maendeleo NORAD, Mamlaka ya Kitaifa ya kudhibiti Ukame Kenya NDMA, na serikali ya Kaunti ya Garasa  kwani kaya zilizoathirika na mafuriko zinapokea msaada wa fedha taslim kupitia M-pesa na vocha za kielektroniki ili kujikimu kimaisha. Flora Nducha anafafanua zaidi katika makala hii

  • UNICEF: Vurugu zinatikisa mfumo wa afya wa Haiti unaoporomoka

    22/05/2024 Duration: 01min

    Ghasia zikiwa zinaongezeka katika mji mkuu wa Haiti, Port-Au-Prince, hospitali sita kati ya kumi nchini humo ziko katika hali mbaya ya utoaji huduma limeonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF.Taarifa ya UNICEF iliyotolewa leo mjini Port-Au-Prince imeeleza kwamba vurugu zimeutikisa mfumo wa afya wa Haiti unaoporomoka kutokana na kwamba makundi yenye silaha yamenyonga minyororo ya usambazaji, na kuweka mamilioni ya watoto katika hatari ya magonjwa na utapiamlo.Kila hospitali nchini Haiti imeripoti ugumu wa kupata na kutunza vifaa muhimu vya matibabu, kwani safari za ndege za kimataifa na za ndani za mizigo kutoka na kwenda katika viwanja vya ndege vya Port-Au-Prince zilirejea kufanya kazi hivi majuzi tu, zikiwa na uwezo mdogo na mrundikano mkubwa, kama ilivyokuwa kwa bandari kuu ambayo hapo awali ilikuwa mikononi mwa makundi yenye silaha."Mfumo wa afya wa Haiti uko karibu kuporomoka," Bruno Maes, Mwakilishi wa UNICEF nchini Haiti amesema akiongeza kwamba, "Mchanganyiko wa vurugu, ufurushaj

page 1 from 5