Habari Za Un

Informações:

Synopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodes

  • Mfumo wa kutoa tahadhari mapema warejesha imani kwa wakazi wa Ituri, DRC

    07/06/2024 Duration: 03min

    Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hususan mashariki mwa taifa hilo la Maziwa Makuu, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umeanzisha mfumo wa kutoa tahadhari mapema kuhusu mashambulizi dhidi ya raia yanayoendeshwa na waasi kwenye mji wa Bunia jimboni Ituri. Mfumo huu unaweza jamii, jeshi la serikali na MONUSCO kubadilishana taarifa na hivyo wananchi wanakuwa na hakikisho la usalama wao kwani pindi taarifa inapotolewa, hatua sahihi zinachukuliwa kama anavyosimulia Assumpta Masso kwenye makala hii iliyofanikishwa na MONUSCO.

  • WHO: Takribani watu milioni 1.6 huugua kila siku kutokana na chakula kisicho salama

    07/06/2024 Duration: 01min

    Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama wa Chakula, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO limeripoti kwamba kila siku, takribani watu milioni 1.6 kote duniani huugua kwa kula chakula kisicho salama na karibu asilimia 40 ya mzigo huo ukibebwa na watoto wadogo, chini ya umri wa miaka mitano. Hii leo kupitia mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari jijini Geneva, Uswisi uliowahusisha Dkt. Francesco Branca, Mkurugenzi wa Idara ya Lishe na Usalama wa Chakula wa WHO na Markus Lipp, Afisa Mwandamizi wa Usalama wa Chakula wa FAO imeelezwa kuwa madhara yatokanayo na chakula kisicho salama hayaangalii mipaka na yametapakaa katika nchi nyingi duniani.  Dkt. Francesco Branca aliyekuwa katika ukumbi huo wa mikutano ametoa taarifa kwamba "kutokana na kuugua kwa takribani watu milioni 1.6 kila siku kunakosababishwa na vyakula visivyo salama, watu 420,000 hufariki dunia kutokana na sababu hiyo."Mwaka huu, kaulimbiu ya kampeni ya Siku ya Kimataifa ya Usalama wa Chakula, ni Jiandae kwa Yasiyotarajiwa,

  • 07 JUNI 2024

    07/06/2024 Duration: 10min

    Hii leo jaridani tunaangazia usalama wa chakula, na ripoti ya ILO kuhusu suala la ajira Gaza wakati huu wa machafuko. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na mashinani tunakupeleka nchini Sudan, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama wa Chakula, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO limeripoti kwamba kila siku, takribani watu milioni 1.6 kote duniani huugua kwa kula chakula kisicho salama na karibu asilimia 40 ya mzigo huo ukibebwa na watoto wadogo, chini ya umri wa miaka mitano. Tukimulika suala la ajira Gaza ambapo ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO inaweka bayana ni kwa vipi vita iliyoanza tarehe 7 Oktoba mwaka jana wa 2023 inasukuma kiwango cha ukosefu wa ajira kufikia takribani asilimia 80 huku pato la ndani la ukanda huo wa Gaza likipungua kwa asilimia 83.5..Katika makala Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa anatupeleka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko masham

  • Vita katika ukanda wa Gaza yasababisha ukosefu wa ajira kufikia asilimia 80 – ILO

    07/06/2024 Duration: 02min

    Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO inaweka bayana ni kwa vipi vita iliyoanza tarehe 7 Oktoba mwaka jana wa 2023 inasukuma kiwango cha ukosefu wa ajira kufikia takribani asilimia 80 huku pato la ndani la ukanda wa Gaza likipungua kwa asilimia 83.5. Takwimu hizo zinamaanisha kuwa kati ya kila watu 10 Ukanda wa Gaza wenye uwezo wa kufanya kazi, ni watu wawili tu wenye ajira, imesema ripoti hiyo iliyoandaliwa na ILO kwa ushirikiano na Ofisi Kuu ya Takwimu ya Palestina kuonesha ni kwa vipi vita imeathiri soko la ajira na njia za kujipatia kipato kwenye eneo hilo la Palestina linalokaliwa na Israeli.Ripoti inasema miezi minane ya vita imesababisha watu kupoteza kwa kiwango kikubwa ajira na mbinu zao za kujipatia kipato Gaza.Ukingo wa Magharibi nako vita hiyo imeathiri vibaya kwani ukosefu wa ajira umefikia asilimia 32.Ripoti inaonya kuwa takwimu hazijumuishi wale waliolazimika kuacha kazi kwa sababu ya vita, na kwamba idadi halisi ya waliolazimika kuacha kazi ni kub

  • Jifunze Kiswahili - Pata ufafanuzi wa neno "Nyendea"

    06/06/2024 Duration: 48s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili  leo Mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania, BAKITA anafafanua matumizi ya neno “NYENDEA”

  • 06 JUNI 2024

    06/06/2024 Duration: 09min

    Katika Jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea -Gaza Nuiserat Israel imeshambulia shule moja iliyokuwa inahifadhi wakimbizi 6,000 wa kipalestina na kuua watu 35, na wengine wengi wamejeruhiwa,-Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa leo kumefanyika tukio la kukumbuka wafanyakazi 188 wa chombo hicho waliouawa mwaka 2023 pekee wakiwemo 135 watumishi wa UNRWA waliouawa ukanda wa Gaza-Duniani kote mtoto mmoja kati ya wanne anaishi katika mazingira ya umaskini wa chakula akila aina moja au mbili tu ya mlo kutokana na vita, mizozo, janga la tabianchi na ukosefu wa uwiano, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF. -Katika mada kwa kina utamsikia Erick Mukiza mmoja wa wanasheria waliothibitishwa kuwa wapatanishi au wasuluhishi wa migogoro nje ya mahakama nchini Tanzania na mipango yake ya kujumuisha wenye ulemavu ili wanufaike na mpango huo wa serikali ya Tanzania.-Na katika jifinze Kiswahili Onni Sigalla anafafanua maana ya nen

  • UN: Kila mtu ana wajibu wa kuhusika na urejeshaji wa ubora wa ardhi

    05/06/2024 Duration: 04min

    Leo ni siku ya mazingira duniani na Umoja wa Mataifa unaisa dunia kuchukua hatua sasa kurejesha Uhai wa ardhi iliyoharibiwa na kujenga mnepo dhidi ya kuongezeka kwa hali ya jangwa na ukame na hiyo ndio kaulimbiu ya siku ya mwaka huu. Akisisitiza maudhui hayo Inger Andersen Mkurugenzi mtendaji wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP amemtaka kila mtu kujiunga na harakati za kimataifa za kurejesha ardhi yenye afya na kujenga mnepo wa majanga mengine kama vile ukame na hali ya jangwa. Flora Nducha anatupasha zaidi katika makala hii..

  • Lengo la kudhibiti ongezeko la joto duniani kwenye nyuzijoto 1.5 linaning’inia - Katibu Mkuu

    05/06/2024 Duration: 02min

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres asubuhi ya leo saa za New York, Marekani kupitia Hotuba Maalumu kuhusu Hatua Dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi ametahadharisha kuhusu hatari ya wazi ya uwezekano wa ongezeko la joto juu ya nyuzijoto 1.5 za selsiasi linaloukabili ulimwengu ikiwa uzalishalishaji wa hewa chafuzi utaendelea kwa viwango vya sasa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Ni hotuba ambayo imepewa jina “Wakati wa Ukweli”…Hotuba ambayo Katibu Mkuu wa Guterres ameitumia kuuleza ulimwengu ukweli kuwa utafiti wa kitaalamu unaonesha kuwa ni tani bilioni 200 tu za hewa ukaa ambazo dunia inaweza kuzihimili kabla ya kuvuka nyuzijoto 1.5 za Selsiasi  juu ya viwango vya kabla ya viwanda jambo ambalo ni hatari kubwa kwa ulimwengu.Ikumbukwe kuwa chini ya Mkataba wa Paris mnamo mwaka 2015, nchi zilikubaliana kupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa hewa chafuzi duniani ili kuwezesha ongezeko la muda mrefu la wastani wa joto la uso wa dunia kuwekwa chini ya nyuzijoto 2 za selsiasi juu ya viwango v

  • 05 JUNI 2024

    05/06/2024 Duration: 10min

    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya mazingira duniani, na msaada wa kibinadamu nchini Haiti. Makala tunamulika hatua za kurejesha afya ya ardhi iliyoharibiwa na mashinani tunasalia hapa makao makuu kusikia ujumbe wa Martin Griffiths anayestaafu mwishoni mwa Juni. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres asubuhi ya leo saa za New York, Marekani kupitia Hotuba Maalumu kuhusu Hatua Dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi ametahadharisha kuhusu hatari ya wazi ya uwezekano wa ongezeko la joto juu ya nyuzijoto 1.5 za selsiasi linaloukabili ulimwengu ikiwa uzalishalishaji wa hewa chafuzi utaendelea kwa viwango vya sasa. Licha ya machafuko na mashambulizi yanayofanywa na makundi yenye silaha huko nchini Haiti, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani limeendelea kuimarisha operesheni zake katika mji mkuu wa Port-au-Prince na kusaidia jamii zilizoathiriwa na ghasia ambapo kwa mwezi Mei shirika hilo limeweza kuwafikia zaidi ya watu 93,000.Katika makala ikiwa leo ni siku ya mazingira duniani

  • WFP yafanikiwa kufikisha Msaada wa chakula nchini Haiti licha ya hali tete ya usalama

    05/06/2024 Duration: 03min

    Licha ya machafuko na mashambulizi yanayofanywa na makundi yenye silaha huko nchini Haiti, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani limeendelea kuimarisha operesheni zake katika mji mkuu wa Port-au-Prince na kusaidia jamii zilizoathiriwa na ghasia ambapo kwa mwezi Mei shirika hilo limeweza kuwafikia zaidi ya watu 93,000. Kwa mujibu wa tathmini ya viwango vya njaa iliyofanyika mwezi Machi mwaka huu nchini Haiti, takriban watu milioni 5 ambao ni sawa na nusu na idadi ya watu wote wa taifa hilo, wanakabiliwa na ukosefu wa uhakika wa chakula ikiwemo watu milioni 1.64 ambao wametajwa kuwa hatua moja tu kabla ya kufikia baa la njaa yani IPC4. Maisha ya wanajamii yamebadilika sana, wale waliokuwa wanaweza kujikimu sasa wamegeuka ombaomba kama anavyoeleza bibi Heugenie Pierre Charles, mwenye umri wa miaka 70 mkazi wa Port- au – Prince. “Kuna wakati mwingine nakuwa na njaa sana. Nawaomba watu wanaokula wanigawie kidogo wanachokula. Lakini wananidhalilisha. Huko nyuma sikuwahi kuwa naomba

  • 04 JUNI 2024

    04/06/2024 Duration: 13min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya ambako UNICEF na wadau wake imefanikisha utengenezaji wa sodo za kufuliwa. Piatunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za Gaza, wahamiaji kutoka bara la Afrika na watoto katika migogoro. Mashinani inatupeleka nchini DR Congo, kulikoni?Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura (OCHA) imeripoti ubomoaji wa makazi leo kwenye eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu katika miji ya Shuqba, Al Jwaya na Mantiqat Shi'b al Butum, katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) imeangazia hatari zinazowakabili wakimbizi na wahamiaji wanapokuwa njiani kutoka Afrika kwenda Ulaya. UNHCR imeweka wazi kuwa wengi wao hufariki dunia wakivuka jangwa au karibu na mipaka, hufanyiwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Shirika hilo limetoa wito kwa wafadhili kuangazia usaidizi na watu kuelezwa njia mbadala halali za kuhama nchi.Na ikiwa le

  • Watumiaji wa baiskeli wasema manufaa ni zaidi ya afya

    03/06/2024 Duration: 03min

    Baiskeli! Umoja wa Mataifa uliitambua rasmi umuhimu wake tarehe 13 mwezi Machi mwaka 2022 kwa kupitisha azimio la kutambua tarehe 3 mwezi Juni kila mwaka kuwa siku ya baiskeli duniani. Umuhimu wake kama chombo cha usafiri chenye gharama nafuu, hakichafui mazingira na zaidi ya yote afya kwa watumiaji kwani ni mazoezi. Huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya, taifa lililo Afrika Mashariki, utamaduni wa kutumia baiskeli kama njia ya usafiri unazidi kushamiri na miongoni mwa watumiaji hao wanaelezea kwenye makala hii msingi wa matumizi, changamoto na nini kifanyike ili matumizi ya baiskeli yawe salama.

  • UNRWA: Gaza hali si hali tena huku watu milioni 1 wakikimbia Rafah

    03/06/2024 Duration: 01min

    Watu milioni moja sasa wamefungasha virago na kuukimbia mji wa Rafah kusini mwa Gaza, ka mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, huku kukiwa na ripoti mpya za mashambulizi ya usiku kuamkia leo katika maeneo ya kusini, kati na kaskazini yanayofanywa na vikosi vya Israel. Katika tarifa yake iliyotolewa leo kupitia mtandao wa kijamii wa X UNRWA imesema mji wa Rafah kwenye mpaka wa kusini wa Gaza na Misri ulikuwa nyumbani kwa zaidi ya watu milioni moja waliokimbia makazi yao kwa karibu miezi minane ya mashambulizi ya kila siku ya jeshi la Israel, kujibu shambulio la kigaidi lililoongozwa na Hamas kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba mwaka jana."Maelfu ya familia sasa wanaishi katika vituo vilivyoharibiwa na kusambaratishwa huko Khan Younis ambapo UNRWA inaendelea kutoa huduma muhimu, licha ya changamoto zinazoongezeka. Masharti hayaelezeki,” Haya yanajiri siku tatu tangu Rais wa Marekani Joe Biden kuzindua pendekezo la usitishaji mapigano kwa kuzingatia usitishaj

  • 03 JUNI 2024

    03/06/2024 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na afya ya uzazi nchini Randa. Mashinani tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Watu milioni moja sasa wamefungasha virago na kuukimbia mji wa Rafah kusini mwa Gaza, ka mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, huku kukiwa na ripoti mpya za mashambulizi ya usiku kuamkia leo katika maeneo ya kusini, kati na kaskazini yanayofanywa na vikosi vya Israel. Nchini Rwanda, hivi karibuni Wizara ya Afya ya nchi hiyo, kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), imeanza usambazaji wa Vidonge vyenye virutubisho vingi vya lishe (MMS) ili kuboresha lishe ya wajawazito kama njia ya kupunguza kasi ya udumavu kwa watoto.Katika makala Umoja wa Mataifa uliitambua rasmi umuhimu wa baiskeli tarehe 13 mwezi Machi mwaka 2022 kwa kupitisha azimio la kutambua tarehe 3 mwezi Juni kila mwaka kuwa siku ya baiskeli duniani. Umuhimu wake kama chombo cha usafiri chenye gharama

  • UNICEF yafanikisha mradi wa Lishe Bora kwa Wanawake Wajawazito nchini Rwanda

    03/06/2024 Duration: 01min

    Nchini Rwanda, hivi karibuni Wizara ya Afya ya nchi hiyo, kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), imeanza usambazaji wa Vidonge vyenye virutubisho vingi vya lishe (MMS) ili kuboresha lishe ya wajawazito kama njia ya kupunguza kasi ya udumavu kwa watoto. Nshimiyimana Clementine, ni Mkuu wa Kituo cha Afya cha Kabaya, Wilayani Ngororero katika Jimbo la Magharibi nchini Rwanda anasema, “Wajawazito wanapata taarifa kutoka kwa Wahudumu Afya Jamii ambao wanawaelekeza kwenda kwenye vituo vya afya kwa ajili ya vipimo muhimu na kupata vidonge vya lishe.”“Tunawashauri kumeza kidonge kimoja kila siku angalau kwa miezi sita. Na sasa kwa kuwa tumeanza kusambaza vidonge lishe hivi tunaamini vitakuwa na manufaa kwa kuzingatia lishe zilizomo. Wajawazito hawatakosa virutubisho kutoka kwenye matunda na mbogamboga kwa kuwa hivi vidonge vinavyo. Japo bado tunawahimiza wajawazito kula matunda na mbogamboga, lakini wale wasiomudu hawataathirika na upungufu wa virutubisho. ”Umugwaneza Yvette ni mmoja w

  • Akili Mnemba inarahisisha mambo lakini inahitaji usimamizi - Profesa Pillay

    31/05/2024 Duration: 03min

    Kila uchao, mikutano ifanyika kona mbali mbali za dunia kubonga bongo ni kwa vipi akili mnemba inaweza kutumika kwa manufaa ya binadamu na si vinginevyo kwani Umoja wa Mataifa unataka nyenzo hiyo iwe ya manufaa hasa katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu. Huko Geneva, Uswisi kumetamatika mkutano wa kujadili ni kwa vipi akili mnemba italeta manufaa. Suala hilo hilo pia lilikuwa miongoni mwa mijadala ya jukwaa la 4 la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali huko Manama, Bahrain ambapo mmoja wa wanajopo alikuwa Profesa Dokta Selvaraj Oyyan Pillay kutoka Malaysia ambaye katika makala hii Assumpta Massoi alizungumza naye na kuumuliza iwapo ana shaka na shuku kuhusu mustakabali wa akili mnemba na nini kifanyika.

  • UNICEF inawasaidia wanafunzi wenye ulemavu wa kutosikia kujifunza kidijitali nchini Kenya

    31/05/2024 Duration: 01min

    Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kupitia mradi unofahamika kama GIGA, kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu, wameunganisha wanafunzi zaidi ya 257,000 kwenye mtandao wa Intaneti, wakiwemo wanafunzi 7,690 wenye mahitaji maalum, na pia mafunzo ya kidijitali kwa maelfu ya walimu.Mmoja wa walimu walionufaika na mafunzo hayo ni Terika Gevera, Mwalimu katika Shule ya Viziwi ya Maseno katika Kaunti ya Kisumu."Wanafunzi wetu mara nyingi hupata ujifunzaji wao kupitia hisia ya kuona, kwa sababu usikivu wao hauwafai sana. Kwa hivyo, UNICEF kuunganisha shule kwenye intaneti kumesaidia sana hasa katika kuboresha ufundishaji wetu. Watoto wetu wanaweza kujifunza na hasa kujifunza kupitia njia ya kuona wanaweza kupata maarifa kwa njia bora zaidi.”Mwalimu Terika Gevera anafafanua zaidi akisema,"Intaneti ni sehemu muhimu sana katika kujifunza. Tuliamunganishwa katika nyenzo za E-Kitabu. E-Kitabu wamejaribu kuandika hadithi zao kwa lugha ya ishara, hivyo wanafunzi hutazama picha, huangalia ishar

  • 31 MEI 2024

    31/05/2024 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Burkina Fasso na mradi unofahamika kama GIGA unaosaidia kufanikisha masomo ya kidijitali kwa wanafunzi nchini Kenya. Makala inamulika usimamizi wa Akili Mnemba na mashinani inatupeleka Garissa nchini Kenya, kulikoni?Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo ameelezea wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la hivi karibuni la mauaji ya raia nchini Burkina Faso, huku kukiwa na madai ya kuwajibika na mauaji hayo kutoka pande zote, makundi yenye silaha na serikali. Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kupitia mradi unofahamika kama GIGA, kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu, wameunganisha wanafunzi zaidi ya 257,000 kwenye mtandao wa Intaneti, wakiwemo wanafunzi 7,690 wenye mahitaji maalum, na pia mafunzo ya kidijitali kwa maelfu ya walimu.Makala inaturejesha Bahrain kufuatilia usimamizi wa Akili Mnemba wakati huu ambapo huko Geneva, wabobezi wa Akili Mnemba na wawakilishi kutoka sekta ya umma na binafsi wakib

  • Volker Türk: Mauaji ya raia Burkina Faso yamefurutu ada lazima yakome

    31/05/2024 Duration: 01min

    Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo ameelezea wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la hivi karibuni la mauaji ya raia nchini Burkina Faso, huku kukiwa na madai pande zote, makundi yenye silaha na serikali kuhusika na mauaji hayo. Kwa mujibu wa tarifa ya ofisi ya Kamishina Mkuu wa haki za binadamu OHCHR kati ya Novemba 2023 na Aprili mwaka huu 2024 imepokea madai ya ukiukwaji wa haki na ukatili unaokiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu ukiwaathiri takriban watu 2732 hili likiwa ni ongezeko la asilimia 71 ya visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu ukilinganisha na miezi sita iliyopita.Taarifa inasema watu 1794 ay asilimia 65 miongoni mwa watu hao ni waathirika wa mauaji ya kinyume cha sheria.Ofisi hiyo ya haki za binadamu imesema Makundi yenye silaha, kama vile Jamāʿat nuṣrat al-islām wal-muslimīn, Kundi kubwa la Kiislamu katika Jangwa la Sahara na makundi mengine yanayofanana na hayo, yamezidisha mashambulizi yao dhidi ya raia, ikiwa ni pamoja na dhidi ya wakimb

  • Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno "Kibuhuti"

    30/05/2024 Duration: 56s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili  leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KIBUHUTI” 

page 1 from 5