Wimbi La Siasa
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 3:57:32
- More information
Informações:
Synopsis
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Episodes
-
Chama tawala nchini Kenya, kwenye njia panda migawanyiko ikishuhudiwa
31/05/2024 Duration: 09minNchini Kenya, malumbano ya kisiasa yameanza kushuhudiwa kati ya rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua, malumbano hayo yametokana na tofauti za kisiasa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2027. Kuna hofu kwamba wandani wa rais William Ruto wanawatumia wabunge vijana kutoka ngome ya naibu rais kumtatiza kisiasa hili likiibua malumbano makli ya kisiasa nchini Kenya.Benson Wakoli hapa anachambua swala hili na mchambuzi wa siasa Felix Arego.
-
Jaribio la mapinduzi nchini DRC lazua maswali mengi
22/05/2024 Duration: 10minWimbi la siasa inaangazia kilichotokea Mei 19 jijini Kinshasa ambako vikosi vya jeshi la serikali (FARDC) viilidai kuzima jaribio la mapinduzi dhidi ya rais wa nchi hiyo.Tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia jumapili ya Mei 19, lakini sasa tukio hilo limeibua maswali mengi bila majibu. Kudadavua hili, utawasikia Georges Msamali, mtaalamu wa masuala ya kiusalama akiwa Nairobi nchini Kenya, Francois Alwende ni raia wa DRC na mtaalamu wa siasa za DRC.
-
Wimbi la siasa: Madai ya Burundi kwa Rwanda kuhusika na vitendo vya uhalifu nchini Burundi
17/05/2024 Duration: 10minKwenye Makala haya Ali Bilali akiwa pamoja na wachambuzi wa siasa Mali Ali kutoka Paris Ufaransa na Abdulkarim Atiki wanaangazi kuhusu tuhuma za Burundi kwa Rwanda kuhusika na vitendo vya uhalifu hususan uvurumishaji guruneti katika mji wa Bujumbura, tukio la hivi karibuni liligharimu maisha ya watu kadhaa na kuwajeruhi wengine.
-
Serikali ya Sudan Kusini na makundi ya waasi yaanza mazungumzo jijini Nairobi
10/05/2024 Duration: 10minMazungumzo ya amani yanayohusisha makundi ya waasi nchini Sudan Kusini na serikali yameanza rasmi jijini Nairobi, wakati huu taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi wa mwezi Disemba. Makundi haya ni yale yaliosusia mkataba wa amani wa mwaka 2018, wakati rais Salva Kiiri na hasimu wa wake wa kisiasa ambaye sasa ni makamo rais wa Kwanza Reik Machar walisaini mkataba wa amani.Soma piaKenya kuisaidia Sudan Kusini kupata suluhu ya utovu wa usalama wa miaka mingiKatika makala haya Benson Wakoli na wachambuzi wa kisiasa Fracis Wambete, ambaye na mhadhiri wa chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda, pamoja na Abdulkarim Atiki, mchambuzi wa siasa za kimataifa kutoka nchini Tanzania wanajaribu kuangazia kufaulu kwa mazungumzo haya, skiza.
-
Nini haki za wafanyakazi duniani ?
01/05/2024 Duration: 10minKila tarehe 1, ni maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani. Wafanyakazi wanatumia siku hii kusherehekea mafanikio yao na kuendeleza mapambano ya haki zao. Je, siku hii ina umuhimu gani ? Wageni wetu ni Nice Mwansasu kutoka Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na mwanasheria wa masuala ya ajira kutoka Kenya Elvis Abenga
-
Mwaka mmoja wa mapigano nchini Sudan kati ya jeshi la serikali na RSF
17/04/2024 Duration: 09minWiki hii, ilikuwa ni mwaka mmoja wa vita nchini Sudan, kati ya jeshi la taifa chini ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na wanamgambo wa RSF wanaongozwa na Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo. Mwaka mmoja baadaye, vita vimeendelea na kusababisha vifo vya maelfu ya watu, huku wengine Milioni 8.5 wakiyakimbia makaazi yao wakiwemo Milioni 1.8 waliokwenda kutafuta hifadhi katika nchi jirani kama Chad.
-
Uhusiano kati ya Somalia na Ethiopia waendelea kuingia baridi
10/04/2024 Duration: 09minWiki iliyopita, Somalia ilimfukuza nchini mwake Balozi wa Ethiopia Mukhtar Mohamed kwa madai kuwa nchi hiyo inaingilia mambo yake ya ndani.Mwezi Januari, mzozo wa kidiplomasia ulianza kushuhudiwa nchini humo baada ya Ethiopia kuingia kwenye makubaliano na jimbo la Somaliland, kutafuta njia ya kufika baharini na kujenga kambi ya jeshi kwenye ukanda wake wa pwani.Nini hatima ya mvutano huu ?
-
Maadhimisho ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda ,ulimwengu umejifunza nini?
03/04/2024 Duration: 09minKumbikizi ya miaka 30 tangu mauaji ya kimbari yaliyosababisha vifo vya watu hadi laki 8 ,kuna wito wa ulimwengu kuhakikisha watuhumiwa zaidi kusakwa na mataifa yaweke mikakati kuzuia mauaji kama haya kutojirudia Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch, sasa linataka jumuiya ya kimataifa kuongeza kasi ya kuwasaka watuhumiwa zaidi wa mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda, ambapo mwishoni mwa juma hili, Kigali itafanya kumbukizi ya miaka 30.
-
Raia wa Senegal wamchagua Faye kuwa rais wao mpya
27/03/2024 Duration: 10minBassirou Diomaye Faye amechaguliwa kuwa rais mpya wa Senegal.Faye mwenye umri wa miaka 44, mshirika wa karibu wa mwanasiasa mwenye ushawishi Ousamane Sonko, ameahidi kufungua ukura mpya wa uongozi wa nchi hiyo.Kwanini raia wa Senegal wamemchagua Faye ? Tunachambua pamoja na Mali Ali akiwa jijini Paris, na Lutege Musa Lutege akiwa jijini Dar es salaam.
-
Makala haya yanatupia jicho uchaguzi wa urais nchini Urusi, nini maana ya ushindi wa rais Vladimir Putin.
20/03/2024 Duration: 10min -
Burundi: Mgawanyiko kwenye chama kikuu cha upinzani CNL
13/03/2024 Duration: 10minNchini Burundi, chama kikuu cha upinzani cha CNL kinashuhudia mgawanyiko baada ya kiongozi wake Agathon Rwasa kuondolewa kwenye nafasi kiongozi wa chama.Hii ilitokea wakati Rwasa akiwa ziarani nchini Kenya.Nini hatima ya kisiasa ya Rwasa ?Tunazungumza naye lakini pia Mali Ali mchambuzi wa siasa za Burundi akiwa jijini Paris.
-
Kenya: Kutuma polisi wake nchini Haiti kuthibiti magenge ya wahalifu
08/03/2024 Duration: 09minSerikali ya Kenya na Haiti zimetiliana saini ili kufanikisha Kenya kutuma polisi wake nchini Haiti kudhibiti magenge ya wahalifu ambayo yameendelea kutatiza usalama nchini Haiti. Katika makala haya Domic Wabala mchambuzi wa usalama na dkt Braine Wanyama, mchambuzi wa siasa za kimataifa wanatathimini nini maana ya Kenya kutuma polisi kule Haiti.
-
Uongozi wa rais wa Sudan Kusini Salva Kiir katika jumuiya ya Afrika Mashariki
28/02/2024 Duration: 10minRais Salva Kiir amekuwa ziarani Rwanda na Burundi kuangazia swala la usalama
-
AU yakosa kupata suluhu kwa mizozo ya Africa
21/02/2024 Duration: 10minViongozi wa Africa wamekutana mwisho wa juma katika mkutano wao wa kila mwaka wa 37, nchini Ethiopia walishindwa kuja na njia ya mapoja kumaliza migogoro barani. Je tatizo la Africa nini?Je Africa inaweza jitegemea? ndio baadhi ya maswali Benson Wakoli, na wachmbuzi mwanadiplomasia Macharia Munene pamoja na mchambuzi wa siasa za kimataifa dkt Braine Wanyama wanajaribu kuyajibu katika makala haya.
-
Wabunge nchini Tanzania wapitisha mageuzi ya sheria za uchaguzi
07/02/2024 Duration: 09minWiki iliyopita, wabunge nchini Tanzania, walipitisha miswada mitatu ya sheria ya uchaguzi kuelekea uchaguzi mkuu mwaka ujao. Tume ya uchaguzi itabadilishwa jina na sasa itafahamika kama Tume huru ya taifa ya Uchaguzi. Mwenyekiti wa Tume na Makamu wake, watateuliwa na rais baada ya kupokea majina matatu kutoka kwenye Kamati ya usaili.Chama kikuu cha upinzani, CHADEMA kinapinga mabadiliko hayo. Wachambuzi wetu ni Mohammed Jawadu akiwa Dar es salaam na Hamdun Marcel akiwa Mwanza.
-
Niger, Mali na Burkina Faso kujiondoa ndani ya ECOWAS
03/02/2024 Duration: 09minMataifa ya Mali, Niger na Burkina Faso, yametangaza kujiondoa kwenye muungano wa ECOWAS, baada ya vikwazo ambayo muungano huu ulitangaza dhidi ya mataifa hayo, kipindi baada ya mapinduzi ya kijeshi. Benson Wakoli pamoja na wachanganuzi wa siasa za kimataifa, dkt Braine Wanyama na Mali Ali, wanatathimini Athari ya Niger, Mali na Burkina Faso kujiondoa ndani ya ECOWAS.Skiza makala haya.
-
Matarajio ya wakongo baada ya kuapishwa kwa rais Félix Tshisekedi
24/01/2024 Duration: 10minWimbi la siasa imeangazia fursa iliyopo kidiplomasia kwa rais wa DRC Felix Thisekedi aliyeapishwa Jumamosi iliyopita, kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili.DR Congo, imekuwa kwenye mvutano wa kidiplomasia na Rwanda, kwa madai kuwa Kigali inawaunga mkono waasi wa M23 eneo la mashariki. Ruben Lukumbuka amewaalika Francois Alwende, mtaalamu wa siasa za DRC akiwa jijini Nairobi pia Guerschome Kahebe pia ni mchambuzi wa siasa akiwa Jijini Washington nchini Marekani.
-
Mvutano kati ya ofisi ya rais nchini Kenya na idara ya mahakama
17/01/2024 Duration: 10minRais wa Kenya William Ruto, ameingia kwenye mvutano na idara ya Mahakama. Ruto anasema Mahakama imejawa na Majaji mafisadi, wanaopindisha haki na kukwamisha miradi za serikali. Jaji Mkuu Martha Koome amekanusha madai hayo. Nini hatima ya mvutano huu ?
-
Mkataba kati ya Ethiopia na eneo lililojitenga na Somalia la Somaliland, kizungumkuti
10/01/2024 Duration: 10minMakala hii imejadili hatua ya rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud kusaini sheria ya kufuta makubaliano kati ya Ethiopia na eneo lililojitenga la Somaliland, hii ikiashiria kutoridhishwa na matumizi ya bandari ya Berbera, uamuzi unaoibua hofu ya kutokea mgogoro baina ya pande hizo mbili.Mwandishi wetu Ruben Lukumbuka ameangazia hili pamoja na mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Washington Marekani, Abdullahi Boru pamoja na profesa Macharia Munene ni mchambuzi wa siasa, na mtaalamu wa maswala ya kidiplomasia akiwa Jijini Nairobi hapa Kenya
-
Utendakazi wa CENI na mrengo wa upinzani katika uchaguzi wa Disemba 20
05/01/2024 Duration: 10minMaandamano yaliotishwa na upinzani kupinga utendakazi wa CENI yalizimwa na polisi nchini DRC