Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle

Informações:

Synopsis

Mission Europe ni somo la lugha lenye sehemu tatu: Mission Berlin, Misja Kraków na Mission Paris. Jitose kwenye bahari ya lugha ujifunze, Kijerumani.

Episodes

  • Mission Berlin 26 – Jaribio la Wakati

    20/03/2009 Duration: 05min

    Anna anapowasili mwaka 2006, anamwambia Paul inawabidi kuukwamisha mtambo. Lakini wanahitaji alama ya siri. Anna anaufuata muziki na mwanamke mwenye mavazi mekundu anawasili. Je atamzuia Anna kutimiza lengo lake? Anna amerejea mwaka 2006 na anamwonyesha Paul ufunguo wenye kutu unaonuiwa kukwamisha mtambo. Hata hivyo mtambo huo unahitaji alama ya siri. Anna anajaribu sauti za muziki DACHFEG. Mwanamke mwenye mavazi mekundu anajitokeza na kumtaka Anna kumpa ufunguo, lakini Anna anautia ufunguo kwenye mtambo na kisha kubonyeza alama ya siri. Je mwanamke mwenye mavazi mekundu atajaribu kuzuia kuharibiwa kwa mtambo? Au atabakia kuwa kumbukumbu, kama mtambo huo ulivyo?

  • Mission Berlin 25 – Vurugu

    20/03/2009 Duration: 05min

    Muda unayoyoma na Anna anamuaga Paul kabla ya kurejea tarehe 9 Novemba mwaka 2006. Atakapowasili atakuwa amebakiwa na dakika tano pekee. Je zitatosha? Huku zikiwa zimesalia dakika chache Anna akamilishe jukumu lake, mchezaji anamshauri kutumia fursa ya zogo lililopo kuondoka pole pole. Lakini hataki kuondoka bila kumuaga Paul sawasawa. Anna anachunguza mchezo na kugundua anahitaji ufunguo uliochakaa kutekeleza jukumu lake. Anaitaji pia muziki. Je atarejea kwa wakati ufaao kutekeleza wajibu wake? Amesalia na dakika 5 pekee ili akamilishe vizuri jukumu lake.

  • Mission Berlin 24 – Saa inayopiga

    20/03/2009 Duration: 05min

    Anna analipata kasha la chuma lililofichwa katika mwaka 1961 lakini hawezi kulifungua kwa kuwa limechakaa. Anapofanikiwa kulifungua anapata ufunguo wa zamani. Je huo ndio ufunguo wa ufumbuzi wa siri? Muda unayoyoma na Anna ni lazima afungue kasha la chuma. Lakini mchezaji anamtahadharisha kutolifungua mbele ya watu. Analifungua kasha hilo na kupata ufunguo wa zamani uliochakaa. Sasa anatakiwa kurudi mwaka 2006 ili akabiliane na mwanamke mwenye mavazi mekundu. Lakini ana muda wa kutosha?

  • Mission Berlin 23 – Tutaonana baadaye

    20/03/2009 Duration: 05min

    Anna anadandia skuta ili afike barabara ya Bernauer. Mhisani wake ni Emre Ogur anayemtakia ufanisi mjini Berlin. Lakini atahitaji nini zaidi kumkimbia mwanamke mwenye mavazi mekundu ili apate kasha la chuma lililofichwa? Mchezaji anamwambia Anna kutafuta usafiri wa kwenda barabara ya Bernauer kwa kuwa muda unamtupa mkono. Anadandia skuta inayoendeshwa na kijana mmoja, ambaye siku za usoni ni Inspekta Emre Ogur. Lakini Anna anapokutana na Heidrun Drei na Paul, mwanamke mwenye mavazi mekundu anawasili.Paul na Robert, mume wake Heidrun Drei, wanamrushia vipande vya ukuta. Wakati huo huo Anna anakimbia kwenda kuopoa kasha la chuma. Lakini je litakuwepo bado baada ya miaka yote hiyo?

  • Mission Berlin 22 – Endelea

    20/03/2009 Duration: 05min

    Anna anapelekwa mwaka 1989 na anafika katika jiji ambalo lina kizaazaa cha kuanguka Ukuta. Anahitajika kupitia umati mkubwa wa watu ili apate kasha la chuma lililofichwa. Je atafanikiwa? Anna anapotaka kuondoka kuelekea mwaka 1989, waendesha pikipiki wanajitokeza. Mwanamke mwenye mavazi mekundu analiamuru kundi lake kumsaka Anna. Anamtaka Anna akiwa hai. Anna anaingia kwenye mtambo wa wakati na anarudi mjini Berlin mwaka 1989 wakati jiji hilo limezama kwenye shamrashamra za kuanguka ukuta. Lakini yuko katika lango la Brandenburg ambapo kila mtu anasherehekea. Anna anapaswa kwenda katika barabara ya Bernauer. Kwa dakika 30 zilizobaki, je anaweza kuharakisha kuuvuka umati wa mamilioni ya watu katika jiji hilo ambalo hapo awali lilikuwa limegawanyika?

  • Mission Berlin 21 – Wakati huo huo mwaka 2006

    20/03/2009 Duration: 05min

    Anna anarejea mwaka 2006 na anagundua, mchungaji Kavalier ametekwa nyara. Kwa kuwa hana uwezo wa kujua aliko mchungaji, Anna anaelekea tisa Novemba, 1989, usiku ambao Ukuta wa Berlin ulianguka. Mwaka 2006, Paul anamwambia Anna kuwa mchungaji ametoweka. Mwanamke mwenye mavazi mekundu amemteka nyara. Paul bila shaka anajua mambo mengi kumuhusu Mchungaji Kavalier na mtambo wa wakati, lakini hana muda wa kuzungumzia hayo. Anna anakubali kuelekea usiku wa tarehe 9 Novemba mwaka 1989 wakati wakazi wa Berlin walipokuwa wakisherehekea kuanguka kwa Ukuta. Anataka kuliopoa kasha kutoka katikati ya kundi la watu.

  • Mission Berlin 20 – Muda baada ya Muda

    20/03/2009 Duration: 05min

    Anna bado hajapata ufumbuzi wa kitendawili chake. Tukio gani la kihistoria RATAVA inataka kuzuia? Mchezaji anamwambia kurejea mwaka 2006 na kisha kurudi tena mwaka 1989. Je harakati hizo zina hatari kiasi gani? Kabla ya Anna kurejea mwaka 2006, anataka kuagana vizuri na Paul. Ana muda wa dakika 35 kukamilisha jukumu lake na inambidi kuchunguza ajue tukio ambalo kundi la RATAVA linataka kusimamisha. Anna na mchezaji wanagundua kuwa kundi la RATAVA halizingatii ujenzi wa ukuta bali kuanguka kwake. Mchezaji anamwambia kwanza arudi mwaka 2006 kisha aende mwaka 1989 wakati ukuta ulipoanguka.

  • Mission Berlin 19 – Mahaba katika hali ya Vita Baridi

    20/03/2009 Duration: 05min

    Zimesalia dakika 40 na Paul na Anna wanamkimbia mwanamke mwenye mavazi mekundu wanafika Berlin Magharibi. Lakini ni upande usioafiki. Mambo yanazidi kutatizika wakati Paul anapomwambia Anna kwamba anampenda. Anna anatakiwa kuwa Berlin Mashariki ili afanikiwe kutekeleza jukumu lake. Lakini amekwama upande wa magharibi. Kisha kuna tatizo jingine: Katika hali ngumu kama hiyo, Paul anamwambia Anna kuwa anampenda. Anamtaka Anna kuacha kutekeleza jukumu lake. Hata hivyo mchezaji anamwambia Anna kurudi mwaka 2006 ili aanzishe mpango mwingine. Dakika 35 zitatosha kupata suluhisho?

  • Mission Berlin 18 – Historia ya kasha

    20/03/2009 Duration: 05min

    Anna anagundua kuwa mwanamke mwenye mavazi mekundu ndiye mkuu wa RATAVA. Dakika 45 zimebaki za kuinusuru Ujerumani na kidokezo alicho nacho Anna ni kasha lililofichwa. Je atalipata na kuweza kukamilisha jukumu lake? Heidrun Drei, Paul na Anna wanaelekea barabara ya Bernauer na njiani wanakutana na Robert, mume wake Heidrun Drei. Anawaarifu kuwa wanajeshi wametapakaa kila mahali: Zaidi ya hayo, wenye pikipiki nao wamejitokeza. Anna na wenzake wanajificha kwenye uwa wa mkahawa wa zamani. Mwanamke mwenye mavazi mekundu anajitokeza na Paul anamwambia Anna kuwa mwanamke huyo ndiye kiongozi wa RATAVA. Mchezaji anamwambia Anna kumfuata kiongozi huyo. Anna na Paul wanakwenda kwenye selo ambako wanamshuhudia mwanamke huyo akificha kasha. Wanachukua kasha lile na kulificha katika sehemu nyingine na kisha kukimbia. Mchezaji anasema atafikiria njia ya kulipata tena. Lakini kwa dakika 40 zilizobaki, atakuwa na muda wa kutosha?

  • Mission Berlin 17 – Kujenga Vizuizi

    20/03/2009 Duration: 05min

    Huku zimesalia dakika 50, mchezaji anasema wakati umefika wa kumwamini keshia. Taarifa ya redio inasema wanajeshi wa Ujerumani Mashariki wanajenga uzuio wa seng'enge. Je hilo ndilo tukio la kihistoria la RATAVA? Anna hajatambua kuwa keshia ni Heidrun Drei na mchezaji anamwambia amwamini keshia huyo anayetaka kumsaidia hata kama kaka yake ana shaka. Hata hivyo ndugu hao wawili wanakubaliana kumsaidia Anna kulikwepa genge la waendesha pikipiki. Wote watatu wanakwenda kuwachungulia wanajeshi wa Ujerumani Mashariki ambao wanaanza kujenga uzio wa seng'enge. Mchezaji anamwambia Anna kuwa huo ni ujenzi wa Ukuta wa Berlin. Zimebaki dakika 45 kuinusuru Ujerumani.

  • Mission Berlin 16 – Nimeuona mustakabali wako

    20/03/2009 Duration: 05min

    Anna anaporudi nyuma hadi mwaka 1961, waendesha pikipiki wenye silaha bado wanamwandama. Mwanamke fulani asiyemjua anamwokoa. Kwa nini akafanya hivyo? Je Anna anaweza kumwamini? Genge la waendesha pikipiki linamwandama Anna. Anajificha kwenye duka la kuuza vyakula na wakati huo huo msimamizi wa duka anamwambia kwamba wakati wa kufunga duka umefika. Msaidizi wake anasema kuwa Anna ni rafiki yake. Keshia huyo anamchukua Anna hadi nyumbani kwake na anamwambia kwamba walisoma pamoja. Nyumbani kwake, keshia anamjulisha Anna kwa Paul Winkler, ambaye ni kaka yake.

  • Mission Berlin 15 – Abiria wa wakati

    20/03/2009 Duration: 05min

    Katika Berlin iliyogawanyika, Anna anapaswa kutoka Mashariki kwenda Magharibi. Hilo silo tatizo la pekee. Ana muda wa dakika 55 kuchunguza lengo la RATAVA. Je ni ujenzi au kubomolewa ukuta? Mwaka 1961, Anna anajaribu kufika Kantstraße. Lakini Kantstraße iko Berlin Magharibi na yeye yuko Berlin Mashariki. Anna hawezi kwenda Magharibi kwa sababu serikali ya Ujerumani Mashariki imeanza kujenga ukuta. Baada ya kuanzishwa upya kwa mchezo, mchezaji na Anna wanagundua kuwa huenda malengo ni mawili: ujenzi au kubomolewa Ukuta wa Berlin. Wanabakiwa na dakika 55 kuchunguza kujua lengo la RATAVA.

  • Mission Berlin 14 – Kurejea siku za usoni

    20/03/2009 Duration: 05min

    Anna anagundua mtambo wa wakati na anaambiwa kuwa genge la magaidi linataka kufuta tukio la kihistoria. Lakini tukio lipi? Mchezaji anamrejesha hadi mwaka 1961. Anasalia na dakika 60. Je amwamini mchungaji? Mchungaji anajua maana ya msemo "In der Teilung liegt die Lösung" na anaelewa hatari ya genge la RATAVA. Mchezaji anasema Anna anapaswa kurudi hadi mwaka 1961 ili kufumbua fumbo hilo. Mchezaji anaahidi atamrejesha Anna alikotoka pindi akifika mwaka huko. Mchungaji anampa msemo "Die Liebe versetzt Berge",…"Mapenzi husogeza milima"… ambao unamsaidia kurejea nyuma. Anaanzia tarehe 13 Agosti lakini akiwa na dakika sitini kutekeleza jukumu lake. Je muda huu unatosha?

  • Mission Berlin 13 – Msaada wa kichungaji

    20/03/2009 Duration: 05min

    Kanisa linakuwa mahali pa kupata mwongozo. Mchungaji anamweleza Anna kuhusu sauti na kwamba sautii hiyo ni ufunguo wa mtambo wa wakati. Lakini anazungumzia kifaa gani? Mchezo unapoanzishwa tena, Anna na mwanamke mwenye mavazi mekundu wanagombana lakini mwanamke huyo anakimbia pindi mchungaji anapowasili. Anamwarifu Anna kwamba Inspekta Ogur amejeruhiwa na anajiuguza hospitalini. Mchungaji anaicheza tena sauti hiyo tena na kumwambia kwamba sauti za muziki D A C H F E G ndizo ufunguo wa mtambo huo. Ugunduzi huo unampa Anna na mchezaji dakika kumi za nyongeza. Lakini muda huo utatosha?

  • Mission Berlin 12 – Muziki wa Kanisa

    20/03/2009 Duration: 05min

    Anna amebakiwa na dakika 65. Anatambua kuwa kikasha cha muziki ndicho sehemu inayokosekana kwenye kinanda cha kanisa. Mwanamke mwenye mavazi mekundu anajitokeza na kudai apewe ufunguo. Ufunguo gani? Anna anasikia wimbo anaoufahamu. Kinanda cha kanisa kinatoa mirindimo sawa na ile ya kwenye kikasha cha muziki. Wakati Anna anapokikaribia kinanda anamsikia mtunza kanisa akimweleza mgeni kuwa kinanda hicho kimerekebishwa ila kinakosa kipande kimoja…ein Element.. tangu ukuta ulipojengwa. Anna anatambua kuwa kikasha ndicho kiungo kinachokosekana na anakibandika kwenye kinanda. Kinanda kinapoanza kupiga, mlango unafunguliwa na anajikuta akiwa amekabiliana na mwanamke mwenye mavazi mekundu. Anatokwa na uhai mwingine na anasaliwa na dakika 60 pekee.

  • Mission Berlin 11 – Mkahawani

    20/03/2009 Duration: 05min

    Anna anamweleza Paul kuhusu msemo usioleweka, "In der Teilung liegt die Lösung. Folge der Musik!" Paul anatambua hatari iliyopo. Anamshauri Anna kumwendea Mchungaji Markus Kavalier. Je pendekezo lake ni sawa? Paul anatambua kuwa sauti iliyopo kwenye kikasha cha muziki haipigi mpaka mwisho wake. Kipande fulani kinakosekana. Anna anamwambia kuhusu ujumbe usioeleweka, "In der Teilun liegt die Lösung; folge der Musik!" Paul anampa "die Spieldose" na anamshauri kwenda kumwona Mchungaji Markus Kavalier katika kanisa la Gethsamane. Mchezaji anamwambia Anna kuwa mahali hapo palikuwa eneo la mikutano ya wapinzani wa utawala wa zamani wa Kikomunisti.

  • Mission Berlin 10 – Kizungumkuti

    20/03/2009 Duration: 05min

    Mchezaji anazijumuisha tarehe 13 Agosti, 1961, siku ya kujengwa ukuta wa Berlin na tarehe 9 Novemba, 1989 wakati ukuta ulipoanguka. Mafanikio ya Anna kwenye jukumu lake yanategemea tarehe hizo. Anna afanye nini? Paul na Anna wanajificha katika duka kubwa la KaDeWe ambako Anna anacheza mchezo wake. Mchezaji anamwambia Anna kuwa ukuta wa Berlin ulijengwa tarehe 13 Agosti, 1961 na ukaanguka tarehe 9 Novemba, 1989. Anna atagundua kuwa ufumbuzi wa fumbo lote hilo ni kugawanywa kwa Berlin.

  • Mission Berlin 09 – Vidokezo vinavyokosekana

    20/03/2009 Duration: 05min

    Anna anakimbia kutoka ukumbi wa maonyesho lakini mwanamke mwenye mavazi mekundu anamuwahi katika duka la Paul. Anna anafanikiwa tena kukimbia na kidokezo kimoja cha fumbo hilo na vipi apate kidokezo kingine? Ogur amemdokeza Anna kuhusu kundi la majambazi la RATAVA . Kwenye duka la saa, Paul Winkler anamwonyesha kwamba amekitengeneza kikasha chake cha muziki. Kinapiga wimbo uitwao "Nostagie" wa Friedrich August Dachfeg. "Ni wimbo wetu", Paul anamwambia Anna lakini Anna haelewi. Ghafla mwanamke mwenye mavazi mekundu anajitokeza na kufyatua risasi. Heidrun Drei anawasili na kupambana na mwanamke huyo ili kuwapa Paul na Anna fursa ya kukimbia. Anna amebakiwa na tarehe mbili: Agosti 13, 1961 na Novemba 9. Lakini mwaka gani?

  • Mission Berlin 08 – Kumaliza udhia

    20/03/2009 Duration: 05min

    Ogur anamwarifu Anna kuhusu mpango muovu wa genge la RATAVA linalotaka kubadilisha historia. Kabla ya kupoteza fahamu, Inspekta Ogur anampa Anna tarehe. Novemba 9. Lakini mwaka gani? Ogur, anayeshuku kuwa Anna amejificha mahali fulani kwenye ukumbi, anamwagiza Anna kutoroka. Mwanamke mwenye mavazi mekundu anampiga Anna risasi na kumtoa uhai mara nyingine. Mchezo unaanzishwa tena na Ogur anamwambia Anna kuwa RATAVA ni kundi la majambazi wanaotaka kubadilisha historia. Ingawa Ogur amejeruhiwa, anampa kidokezo cha tarehe, Novemba 9. Lakini mwaka gani?

  • Mission Berlin 07 – Maadui wasiojulikana

    20/03/2009 Duration: 05min

    Anna analikwepa genge la waendesha pikipiki na kuingia kwenye ukumbi wa maonyesho. Huko anakutana tena na Heidrun, na Ogur anamwambia kuwa RATAVA wanamwandama. Lakini wanamtakia nini? Mchezaji anamwambia Anna kurejea dukani kwa Paul Winkler kuchukua kikasha chake cha muziki. Njiani inambidi kulikwepa genge la waendesha pikipiki kwa kuingia kwenye ukumbi wa maonyesho. Huko anakutana tena na Heidrun Drei. Inspeka Ogur anawasili kumhoji Heidrun Drei kuhusu aliko Anna. Ogur anakisia kuwa Anna kajificha kwenye ukumbi huo na anamtahadharisha kwamba genge la RATAVA linamwandama. Wakati huo mwanamke aliyevalia mavazi mekundu anawasili.

page 1 from 2