Siha Njema

Informações:

Synopsis

Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.

Episodes

  • Ajali za barabara Afrika huchangiwa na utepetevu, kasi na msongo wa mawazo

    23/04/2024 Duration: 10min

    Ajali za barabara huchangia vifo vingi vya watu walio katika umri kati ya miaka mitano hadi 29 kwa mujibu wa WHO Uchunguzi unaofanywa baada ya ajali huonesha madereva wengi hulaumi kufeli kwa breki ilhali wengi wana msongo wa mawazo ,imesema mamlaka ya usalama barabarani nchini Kenya ,National Transport and Safety Authority. Ongezeko la magari,mchipuko wa miundo mbinu bora na ongezeko la watu yanazidi kufanya uwezekano wa mtu kuhusika kwenye ajali  kuwa mkubwa.

  • Watu wengi wanajikuta na magonjwa ya figo na ini,watoto wengi Sudan wakiaga

    17/04/2024 Duration: 10min

    Kuna ongezeko la magonjwa ya figo na ini kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO inabashiri kuwa ongezeko hilo litakuwa juu zaidi kufikia mwaka 2030 ,hali hii ikichangiwa na hali ya maisha haswa ya raia katika nchi zinazoendeleaUgonjwa wa ini maarufu Hepatitis pia ni tishio kubwa haswa kwa raia wa Afrika ambayo inachangia asilimia 63 ya visa vya HepatatisNchini Sudan watoto wengi haswa walio chini ya umri wa miaka mitano wanazidi kupoteza maisha kutokana na utapiamlo unaohusishwa na ukosefu msaada  wa kibinadaam wakati huu vita vikiendelea kurindima

  • Uhitaji wa huduma za dharura za afya washika kasi ukanda wa Afrika

    10/04/2024 Duration: 09min

    Shirika la AMREF Flying doctors linaonya kuwa mlipuko wa magonjwa yasiyoambukizwa yanazidi kuongeza uhitaji huku wigo la kupanua biashara likitanuka pia

  • Wanawake waongoza juhudi za kampeni za Afya bora ,DRC ikizidisha mapambano ya Kipindu Pindu

    02/04/2024 Duration: 09min

    Wawawake kutoka ukanda wa Afrika wanajumuika Dar  Es Salaam  mwishoni mwa juma kupiga jeki kampeni za kuboresha afya Nchini DRC mikakati iliyoweka kudhibiti mlipuko wa Kipindu Pindu ulioripotiwa katika mataifa ya Afrika ya Kusini ,inaendelea kulipa na hata kuwa msaada kwa mataifa jirani kama vile Zambia

  • Mataifa ya Afrika yanayoendelea bado yanachangia mzigo mkubwa wa TB

    29/03/2024 Duration: 10min

    Usalama mdogo nchini Sudan Kusini umesababisha wagonjwa wengi kuchelewa kubainishwa TB na kupata matibabu ya mapema Watalaam wa afya wanashauri ulimwengu kukumbatia teknolojia za kisasa kama vile Akili Mnemba kurahisisha ubainishaji na kuongeza usahihi wa vipimo

  • Wanawake mbele kuinua sekta ya sayansi na utafiti nchini Kenya

    13/03/2024 Duration: 10min

    Idadi ya wanawake wanaongoza katika sekta mbali mbali bado ni ndogo barani Afrika. Kauli mbinu mwaka huu wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake ni kuwekeza zaidi kwa wanawake ili kuongeza kasi ya maendeleo,tunaangazia wanawake wanasayansi na watafiti nchini Kenya ,wakijikita kwenye utafiti wa magonjwa yaliyotengwa

  • Jamii ya Kibera jijini Nairobi inavyopambana na mimba za utotoni

    10/03/2024 Duration: 10min

    Mimba za utotoni ni kizingiti kikubwa kinachoathiri elimu ya wasichana barani Afrika

  • UNITAID mbioni kurahisisha upatikanaji wa dawa nadra sokoni

    28/02/2024 Duration: 09min

    UNITAID imekuwa ikishirikiana na mataifa kuleta dawa mpya na za bei nafuu Upatikanaji wa dawa zilizo za viwango vya juu na kwa bei nafuu bado ni changamoto kubwa kwa mataifa yanayoendelea.Matibabu ambayo bado ni mapya hukumbwa na vikwazo vingi kuingia soko la kimataifa na sasa UNITAID imekuwa mbioni kuziba pengo hilo

  • Ushirikiano kati ya shirika la Village Reach na wizara ya afya nchini Kenya na nchi za ukanda wa Afrika

    06/02/2024 Duration: 10min

    Village Reach ambayo kwa tafsiri rahisi ni kufikia maeneo ya vijijini, imefungua ofisi za kikanda jijini Nairobi kujaribu kusaidia serikali kusimamia namba ya dharura,usafirishaji wa sampuli za Polio na kuboresha utendakazi wa wahudumu wa afya wanaofanya kazi katika jamii tofauti Baada ya kupata mafanikio makubwa katika nchi za Msumbiji, Malawi ,Village Reach inapanga kutumia mafunzo hayo kusaidia kuboresha huduma za afya katika mataifa ya Afrika.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ,Village reach imeimarisha huduma za utoaji chanjo ,usafirishaji wa chanjo kutumia ndege zisizo na rubani katika maeneo yasiyo na miundo mbinu ikiwemo mkoa wa Equateur.Aidha shirika hilo linatoa huduma kwa ushirikiano na serikali katika mataifa mengine yenye mzozo kama vile Niger na Sudan Kusini.Afisa mkuu mtendaji Emily Bancroft amesisitiza mifumo ya afya inastahili kuwa thabiti ili kuwa na uwezo wa kustahimili majanga na hali za dharura kama ilivyoshuhudiwa wakati wa Uviko 19

  • Changamoto za afya ya akili katika mitaa ya mabanda nchini Kenya

    24/01/2024 Duration: 09min

    Shirika la afya duniani limeorodhesha ongezeko la watu wanaokumbwa na changamoto za afya ya akili hususan tangu kuzuka janga la Corona,kupanda gharama ya maisha na mfumuko wa bei 

  • Mikakati kuboresha matibabu ya TB

    15/01/2024 Duration: 08min

    Juhudi zinaendelea kuhakikisha dawa mwafaka ya TB miongoni mwa watoto zinaendelea Licha ya kuwa TB inaweza kuambukiza watu wa umri wowote ,watoto kwa miaka wamekuwa wakiachwa nyuma katika matibabu ya TB. Watoto kwa miaka walilazimika kutumia donge za watu wazima.

  • Muendelezo wa ugonjwa wa Kisukari nchini Kenya na Sudan Kusini

    05/01/2024 Duration: 09min

    Nchi zinazoendelea zinashuhudia ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa ukiwemo Kisukari

  • Wadau wa afya wapaza sauti kuhusu ongezeko la magonjwa tengwa wakionya ni tishio katika mifumo ya afya

    22/12/2023 Duration: 10min

    Wadau katika sekta ya afya wana wasi wasi kuhusu ongezeko la magonjwa yaliyotengwa ambayo mengi yao hayana tiba au matibabu yao hayapatikani kwa urahisi au ni bei juu Wawekezaji katika sekta ya uzalishaji dawa ,chanjo hawavutiwi kuzitengeneza dawa za magonjwa hayo. Magonjwa hayo ni kama vile ugonjwa wa malale,matende ,Chikukungunya  na Dengue.

  • Matumizi ya Akili mnemba au AI kuboresha huduma za Afya

    22/12/2023 Duration: 10min

    Ulimwengu umeanza kukumbatia matumizi ya akili mnemba au AI kuboresha huduma muhimu licha ya kuwa bado kukamilika mchakato wa kudhibiti matumizi ya teknolojia hiyo. Katika sekta ya afya mfumo wa AI umeanza kutumika kwenye ubainishaji wa magonjwa na ufuatiliaji wa matibabu.

  • Ugonjwa wa Utindio wa Ubongo almaarufu Celebral Palsy

    22/12/2023 Duration: 10min

    Ugonjwa unaofahamika kama Utindio wa ubongo au Cerebral Palsy kwa lugha ya kimombo ni ugonjwa unaoathiri ubongo, namara nyingi  unatokea kwa watoto na husababishwa wakati damu inapovuja kwenye ubongo au hakuna hewa yakutosha.Unaweza kutokea wakati Mtoto anapoanza kupoteza fahamu punde baada ya kuzaliwa au mwezi wa kwanza wa kuzaliwa.Vilevile Jeraha kwenye ubongo linaweza kusababisha matatizo ya kuongea na ugumu wa kufahamu mambo.Sikiliza makala haya kutambua zaidi kuhusu ugonjwa huu.

  • Afya ya umma barani Afrika

    01/12/2023 Duration: 09min

    Kongamano la tatu la CPHIA kuhusu huduma za afya barani Afrika.

  • Mpango wa afya kwa wote barani Afrika

    21/11/2023 Duration: 10min

    Mataifa mengi yana matamanio ya kuhakikisha raia wake wanapata huduma bora za afya kwa bei nafuu,safari hii ikiwa bado ina panda shuka kwa mataifa mengi. Huduma za afya barani Afrika  zina mfungamano na hali ya kisiasa,uchumi  na pia utawala bora.

  • Faida za mazoezi ya Yoga kwenye mwili wa mwanadamu

    16/11/2023 Duration: 10min

    Yoga ni mazoezi ya mwili yanayoongeza nguvu kwa misuli na kunyoosha  mifupa lakini pia yoga inalenga kuunganisha mwili, ufahamu, na akili kwa pamoja. Hivyo ni tofauti kabisa na aina nyingine za mazoezi.Sikiliza makala haya kwa ufahamu zaidi.

  • Ongezeko la visa vya mdomo Sungura

    03/11/2023 Duration: 09min

    Watalaam wanahofu kuhusu ongezeko la watoto wanaozaliwa na mdomo sungura au Cleft Clip Licha ya kuwa utafiti haujabainisha moja kwa moja sababu ya mdomo sungura ,lishe,urithi na matumizi ya sigara zimetajwa kuchangia hali hii

page 1 from 2