Sbs Swahili - Sbs Swahili

Makala leo:mkataba wa muungano wa falepili kati ya australia na tuvalu wazinduliwa rasmi

Informações:

Synopsis

Mkataba wa Muungano wa Falepili kati ya Australia na Tuvalu uliangaziwa kama wa kwanza wa aina yake duniani, ukiwa na kifungu kimoja cha makubaliano kinachoruhusu hadi watu 280 wa Tuvalu kuhamia Australia kila mwaka kama njia ya kukabiliana na viwango vya bahari vinavyoongezeka na kutishia ardhi yao. Kikundi cha kwanza cha wahamiaji chini ya makubaliano haya sasa wamewasili Australia. Hata hivyo, pamoja na kuwepo kwa jamii ndogo ya watu wa Tuvalu huko, wanakabiliwa na changamoto ya kuzoea makazi mapya, huku wakidumisha uhusiano na jamii na utamaduni wao.