Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Akina mama wahifadhi mashamba ya pweza Lamu katika bahari hindi

Informações:

Synopsis

Sote tunataka familia zetu ziwe na chakula cha kutosha ili kula kile ambacho ni salama na chenye lishe. Na lengo la 2 la maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ni ulimwengu usio na njaa ifikapo 2030.  Lakini licha ya juhudi zinazowekwa, suala la njaa na uhaba wa chakula limeonyesha ongezeko la kutisha tangu 2015, hali hii ikichochewa na mseto wa mambo ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na upungufu wa uzalishaji wa chakula.Kisiwani Pate jimboni Lamu, hapa akina mama wana zaidi ya mashamba matatu ya pweza katika bahari hindi, kwa manufaa ya chakula na mapato.