Jukwaa La Michezo

Informações:

Synopsis

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali. 

Episodes

  • Timu za Afrika zaanza kutangaza vikosi kuelekea AFCON 2024

    30/12/2023 Duration: 23min

    Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa vikosi vya mwisho vilivyotangazwa na mataifa kadhaa kuelekea AFCON ya mwaka 2023 itakayoanza Januari 13, 2024, raia wa Rwanda Clare Akamanzi ateuliwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa NBA Africa, Guy Bukasa atangazwa kocha mpya wa AS Kigali, rais wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach atangaza mikakati ya kujumuisha michezo ya kielektroniki e-sports kwenye Olimpiki na kocha Carlo Ancelotti atia saini mkataba mpya klabuni Real Madrid.

  • Kenya yaibuka bingwa wa mashindano ya Tong Il Moo Do

    23/12/2023 Duration: 23min

    Tuliyokuandalia ni pamoja na Kenya kuhifadhi taji lake la Tong Il Moo Do kwa mara ya 11, mkenya Angella Okutoyi ashinda dhahabu mbili kwenye tenisi ya kimataifa ya W25, uchambuzi wa matokeo ya mechi za Klabu bingwa Afrika wiki hii, Man City kutwaa ubingwa wa Kombe la Klabu bingwa Duniani kwa mara ya kwanza na Mahakama ya Ulaya kupinga uamuzi wa FIFA na UEFA kuzuia kuanzishwa kwa Ligi mpya ya Ulaya kuwa kinyume na sheria. 

  • Mashindano ya Kimataifa ya Tong-Il-Moo-Do yafanyika nchini Kenya

    16/12/2023 Duration: 21min

    Kenya yaandaa makala ya 11 ya michuano ya kimataifa ya mchezo wa Tong-Il-Moo-Do jijini Mombasa. Uganda ndio washindi wa CECAFA katika mechi za kufuzu kwa michuano ya CAF ya Shule za Afrika. Al Ahly waishinda Al-Ittihad kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu Kisha Paris Saint - Germain yatinga hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa.

page 2 from 2