Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 8:01:59
  • More information

Informações:

Synopsis

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.

Episodes

  • Rais Ruto aibua hisia kali kwa kuwaagiza polisi kuwapiga risasi ya miguu waandamanaji

    12/07/2025 Duration: 20min

    Wiki hii watu wasiopungua 38 waliuawa nchini Kenya kufuatia maandamano ya SabasAba siku ya Jumatatu. Rais Ruto aliibua hisia kali alipowaagiza polisi kuwapiga risasi ya miguu waandamanaji. Lakini pia, malalamiko yaliwasilishwa rasmi huko Brussels, dhidi ya wanafamilia tisa wa rais wa DRC Félix Tshisekedi, ambao wana uraia wa Ubelgiji, wakituhumiwa kwa wizi wa madini ya nchi yao. Tutakujuza pia taarifa za kikao cha Rais wa Marekani Donald Trump na marais sita wa Afrika magharibi kilichofanyika, lakini pia Uingereza na Ufaransa kutangaza rasmi mpango wa majaribio wa kuwarudisha Paris baadhi ya wahamiaji wanaowasili nchini humo kwa kutumia boti ndogo.

  • Rais Kagame na Makubaliano ya Washington DC na mazishi ya Albert Ojwang Kenya

    05/07/2025 Duration: 20min

    Yaliyoangaziwa katika makala hii ni pamoja na kauli ya rais wa Kenya kujenga kanisa ndani ya ikulu ya Nairobi, rais Paul Kagame wa Rwanda na mkataba wa amani ulioisainiwa kati ya nchi yake na DRC, waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa kutogombea tena ubunge kuwakilisha jimbo la Ruangwa, hali nchini DRC, Sudan na kauli ya Ufaransa kuwa inatarajia Algeria kumsamehe mwandishi wa vitabu Boualem Sansal aliyefungwa, lakini pia mkutano wa viongozi wa Ulaya kule London Uingereza kufanyika wiki ijayo

  • Maandamano mapya yaua 16 Kenya, DRC na Rwanda zasaini makubaliano ya amani

    28/06/2025 Duration: 20min

    Wiki hii ulimwengu umeshuhudia matukio mengi ya ajabu na hatari sana kwa usalama wa nchi mbali mbali, kwanza nchini Kenya watu 16 waliuawa katika maandamano ya kuadhimisha mwaka mmoja wa mauaji ya vijana Gen Z, Rwanda na DRC zatia saini mkataba wa amani kumaliza vita vya mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, siasa za Chad, Zambia na pia mashambulizi kati ya Israeli na Iran, pamoja na mkutano wa jumuia ya NATO..na mengine mengi

  • Israeli na Iran zaendelea kushambuliana, matukio mengine duniani

    21/06/2025 Duration: 20min

    Mashambulio makubwa kwa makombora kati ya Israeli na Iran, na hali inayoendelea hadi sasa, maandamano ya kupinga kifo cha mwanablogu Albert Ojwang yaliyofanyika baada ya naibu Inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat kutangaza kujiuzulu nafasi kupisha uchunguzi, hali ya kisiasa nchini DRCbaada ya waziri wa sheria Constant Mutamba kujiuzulu, na vile vile siasa za ukanda wa Afrika mashariki, Afrika ya magharibi na kaskazini na kwengineko duniani.-

page 2 from 2